• HABARI MPYA

  Tuesday, March 15, 2016

  TFF YAREKEBISHA TENA RATIBA LIGI KUU

  RATIBA MPYA LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA;
  Machi 16, 2016
  Azam FC Vs Stand United
  Machi 18, 2016
  Kagera Sugar Vs Mtibwa Sugar
  Machi 19, 2016
  Coastal Union Vs Simba SC
  Majimaji Vs Mbeya City
  Stand United Vs Ndanda FC
  Machi 20, 2016
  African Sports Vs Prisons
  Machi 21, 2016
  Mgambo JKT Vs Toto Africans
  Machi 24, 2016
  African Sports Vs Toto Africans
  Aprili 2, 2016
  Majimaji Vs Simba SC
  Yanga SC Vs Kagera Sugar
  Toto Africans Vs Azam FC
  Stand United Vs Mgambo JKT
  Ndanda FC Vs Prisons
  Mbeya City Vs Coastal Union
  Aprili 3, 2016
  JKT Ruvu Vs African Sports
  Mwadui FC Vs Mtibwa Sugar
  Aprili 5, 2016
  Toto Africans Vs Yanga SC
  Azam FC Vs Ndanda FC
  Aprili 9, 2016
  Stand United Vs Yanga SC
  Ndanda FC Vs Mwadui FC
  Na Somoe Ng’itu, DAR ES SALAAM
  YANGA haitacheza mechi yoyote ya Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara mwezi huu, wakati wapinzani wao katika mbio za ubingwa, Simba na Azam watacheza mechi moja moja.
  Kwa mujibu wa marekebisho ya Ratiba ya Ligi Kuu yaliyotolewa leo, Azam FC watacheza na Stand United kesho Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, wakati Simba SC watacheza na Coastal Union Jumamosi Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. 
  Bodi ya Ligi imelazimika kufanya marekebisho ya Ratiba ya Ligi Kuu kupisha ratiba ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars katika mechi za kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika 2017.
  Taifa Stars itakuwa na mchezo wa kufuzu AFCON Kundi G dhidi ya Chad mjini N’jamena Machi 25, kabla ya timu hizo kurudiana Machi 28, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Na baada ya mechi za mwishoni mwa wiki za michuano ya klabu barani, Afrika wachezaji wa Stars wanatarajiwa kukusanywa Jumapili kabla ya safari Jumanne kuelekea Chad.
  Yanga SC baada ya ushindi wa 2-1 kwenye mchezo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya APR Jumamosi mjini Kigali, watarudiana na timu hiyo ya jeshi la Rwanda Jumamosi wiki hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Na Azam FC baada ya kushinda 3-0 mjini Johannesburg, Afrika Kusini dhidi ya wenyeji Bidvest Wits katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza Kombe la Shirikisho Afrika, watarudiana na timu hiyo Jumapili, Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Ligi Kuu itaendelea Aprili 2, kwa Yanga kumenyana na Kagera Sugar Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Simba SC kumenyana na Majimaji Uwanja wa Majimaji mjini Songea, wakati Azam FC watakuwa wageni wa Toto Africans Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TFF YAREKEBISHA TENA RATIBA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top