• HABARI MPYA

  Tuesday, March 15, 2016

  DRC WAJITOA AFCON ZA U17 NA U20

  JAMHURI ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imejitoa kwenye michuano ya kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 na miaka 20.
  Shirikisho la Soka DRC (FECOFA) limetuma taarifa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) juu ya kujitoa kwenye mechi za kufuzu za U-17 na U-20 kwa ajili ya fainali za Afrika mwakani.
  Kwa matokeo hayo, Burundi waliopangwa kumenyana na DRC katika Raundi ya Kwanza kuwania tiketi ya AFCON ya U-20 nchini Zambia mwaka 2017 wamefuzu bila jasho kwenda Raundi ya Pili.
  Na Chad iliyopangwa kucheza na DRC Raundi ya Kwanza kuwania tiketi ya AFCON ya U-17 nchini Madagascar 2017, imefuzu Raundi ya Pili.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DRC WAJITOA AFCON ZA U17 NA U20 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top