• HABARI MPYA

  Tuesday, March 15, 2016

  CAPTAIN AYOUB WA SIMBA AFARIKI DUNIA

  KOCHA na mchezaji wa zamani wa Simba, Ayuob Mohammed maarufu kama 'Captain' amefariki dunia.
  Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba, Hajji Sunday Manara amesema kwamba Captain Ayoub amefariki dunia leo asubuhi nyumbani kwake Mwananyamala B na mazishi yake yanatarajiwa kuwa kesho Alasiri huko huko Mwananyamala, Dar es salaam.

  Captain Ayoub wa tatu kulia waliosimama akiwa na kikosi cha Tanganyika miaka ya 1950

  Manara amesema kwamba Captain Ayuob licha ya kuichezea Simba enzi hizo ikiitwa Sunderland, pia aliichezea kwa muda mrefu timu ya taifa ya Tanganyika huku akiwa Nahodha wa timu zote (Sunderland na Tanganyika).
  Captain Ayuob alikuwa Kocha Msaidizi wa marehemu Paul West Gwivaha walipoiwezesha Simba kuifunga Mufurila Wonderes mabao 5-0 kwao nchini Zambia, baada ya awali timu hiyo kuwafunga Wekundu wa Msimbazi 4-0 Dar es Salaam katika Klabu Bingwa Afrika mwaka 1979.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CAPTAIN AYOUB WA SIMBA AFARIKI DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top