• HABARI MPYA

  Sunday, March 13, 2016

  SALADIN SAID AREJESHWA KIKOSINI ETHIOPIA KWA AJILI YA ETHIOPIA

  MSHAMBULIAJI Saladin Said (pichani kushoto) amerejeshwa kwenye kikosi cha Ethiopian kwa mara ya kwanza baada ya miezi tisa kwa ajili ya mechi mbili za kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2017 dhidi ya Algeria, baadaye mwezi huu.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 amejiunga na klabu ya nyumbani, St. George baada ya kuvunja Mkataba wake na MC Alger ya Ageria mwezi Januari na aliichezea mara ya mwisho kikosi cha Walia katika mchezo wa ufunguzi wa kufuzu dhidi ya Lesotho nyumbani Juni mwaka jana akifunga bao la ushindi wa 2-1.
  Mshambuliaji huyo mzoefu ni miongoni mwa wachezaji maarufu katika kikosi cha awali cha wachezaji 24 waliotajwa na kocha  Yohannes Sahle wikin iliyopita. 
  Walia watasafiri kwenda Blida kwa mechi za tatu za Kundi J itakayopigwa Ijumaa ya Machi 25, kabla ya timu hizo kurudiana siku nne baadaye Addis Ababa.
  Kikosi kamili cha Ethiopia kinaundwa na makipa; Abele Mamo (Mugher Cement), Lealem Birhanu (Sidama Coffee), Tarike Getenet (Dedebit)
  Mabeki: Seyoum Tesfaye (Dedebit), Alula Girma (Saint George), Tekalegn Dejene (Dedebit), Souliman Mohammed (Adama City), Asechalew Tamene (Saint George), Anteneh Tesfaye (Sidama Coffee), Yared Bayeh (Dashen Beer),Wendifraw Getahun (Ethiopian Coffee)
  Viungo: Gatoch Panom (Ethiopian Coffee), Asrat Megeressa (Dashen Beer), Biniam Belay (Commercial Bank of Ethiopia), Tadele Mengesha (ArbaMinch City), Behailu Assefa (Saint George), Shemeles Bekele (Petrojet, Egypt), Elias Mamo (Ethiopian Coffee),  Ramkel Lok (Saint George)
  Washambuliaji: Dawit Fikadu (Dedebit), Getaneh Kebede (University of Pretoria, South Africa), Tafesse Tesfaye (Adama City), Mulualem Tilahun (Defence Force), Salahdin Said (Saint George).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SALADIN SAID AREJESHWA KIKOSINI ETHIOPIA KWA AJILI YA ETHIOPIA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top