• HABARI MPYA

    Wednesday, March 16, 2016

    PWANI WAINGIA VITANI JKT RUVU ISISHUKE

    Na Somoe Ng'itu, DAR ES SALAAM
    WADAU mbalimbali wa soka wa mkoa wa Pwani wameungana na uongozi wa timu ya JKT Ruvu kuhakikisha klabu hiyo ya jeshI inabaki kwenye Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara msimu ujao.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE jana, Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Pwani, Hassan Othman 'Hassanoo' alisema kwamba wamekutaka na kupanga mikakati mbalimbali ya kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri mechi zake zilizobakia kwenye ligi hiyo.
    Kikosi cha JKT Ruvu kinachopambana kuepuka kushuka daraja
    Hassanoo alisema kwamba hatua ya kwanza ilikuwa ni kuiridisha kwenye Uwanja wake wa Mabatini ulioko katika eneo la Mlandizi mkoani humo na wanashukuru Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kukubali ombo lao.
    " Hatutakubali kuona timu yetu inashuka daraja, mkakati wa kwanza ulikuwa ni kuona Ruvu Shooting inarejea na huo umekamilika, sasa tunapambana usiku na mchana, ndani na nje ili tubaki Ligi Kuu," alisema Hassanoo.
    Baada ya kurejea Mabatini kutoka kwenye Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam, JKT Ruvu inayofundishwa na Abdallah 'King' Kibadeni ilishinda mechi mbili nyumbani kwake dhidi ya Toto Africans (2-0) na ikaifunga Mwadui FC bao 1-0.
    Timu hiyo sasa iko katika nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 21 na ikibakiza mechi mbili kwenye uwanja wake wa nyumbani dhidi ya Ndanda FC na Stand United.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PWANI WAINGIA VITANI JKT RUVU ISISHUKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top