• HABARI MPYA

  Saturday, March 19, 2016

  PLUIJM AWAPANGIA APR KIKOSI CHA HAWATOKI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KAMA ilivyotarajiwa, Kocha Mholanzi wa Yanga, Hans van der Pluijm amemuanzisha beki Mkongo Mbutu Twite katika nafasi ya Juma Abdul upande wa kulia wa Uwanja.
  Mbuyu Twite atacheza beki ya kulia leo katika mchezo wa marudiano Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika, badala ya Juma Abdul Jaffar ambaye atakuwa anatumikia adhabu ya kadi za njano mfululizo 
  Mfungaji huyo wa bao la kwanza katika ushindi wa 2-1 kwenye mchezo wa kwanza Jumamosi iliyopita mjini Kigali, alipewa kadi katika mechi mbili mfululizo zilizopita dhidi ya Cercle de Joachim ya Mauritius na APR.
  Katika kikosi hiki anakosekana Juma Abdul tu (katikatib walioinama) ambaye nafasi yake imechukuliwa na Mbuyu Twite

  Lakini Pluijm amewarudisha wachezaji wengine 10 wote walioanza Kigali, ambao ni kipa Ally Mustafa ‘Barthez’, mabeki Mwinyi Hajji Mngwali, Kevin Yondan, Vincent Bossou, viungo Pato Ngonyani, Thabani Kamusoko katikati, Deus Kaseke na Haruna Niyonzima wataocheza pembeni.
  Utaona Pluijm ameendelea kumtumia beki Ngonyani kama kiungo mkabaji ili kuimarisha ukuta, wakati washambuliaji ni Amissi Tambwe na Donald Ngoma.
  Katika benchi wapo Deo Munishi ‘Dida’, Salum Telela, Oscar Joshua, Godfrey Mwashiuya, Paul Nonga, Malimi Busungu na Simon Msuva.
  Sare yoyote ni nzuri kwa Yanga na watasonga hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika na ikitokea bahati mbaya ya kufungwa 1-0 pia watafuzu.
  Wakifungwa 2-1 mchezo utahamia kwenye mikwaju ya penalti, lakini wakifungwa 3-2 watatolewa kwa mabao ya ugenini baada ya matokeo ya jumla kuwa 4-4, lakini APR watasonga mbele kwa kufunga mabao mengi ugenini.
  Mshindi wa jumla atakutana na mshindi kati ya Al Ahly ya Misri na Recreativo de Libolo ya Angola katika 16 Bora. 
  Kikosi cha APR cha Yanga leo; Ally Mustafa ‘Barthez’, Mbuyu Twite, Mwinyi Hajji Mngwali, Kevin Yondan, Vincent Bossou, Pato Ngonyani, Thabani Kamusoko, Deus Kaseke, Donald Ngoma, Amissi Tambwe na Haruna Niyonzima
  Benchi; Deo Munishi ‘Dida’, Salum Telela, Oscar Joshua, Godfrey Mwashiuya, Paul Nonga, Malimi Busungu na Simon Msuva.
  APR huenda wakaanza hivi; Olivier Kwizera, Rusheshangoga Michael, Rutanga Eric, Rwatubyaye Abdul, Bayisenge Emiry, Yannick Mukunzi, Fiston Nkinzingabo, Benedata Janvier, Bigirimana Issa, Iranzi Jean Claude na Sibomana Patrick.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PLUIJM AWAPANGIA APR KIKOSI CHA HAWATOKI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top