• HABARI MPYA

    Friday, March 18, 2016

    MAREFA WA BONGO WAPEWA KAZI CAF

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya waamuzi watakaochezesha na kusimamia michezo ya Kombe la Shirikisho Afrika (CC), kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika (AFCON) pamoja na kuwania kufuzu kwa Fainali za Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 (U20) mwaka 2017.
    Michael Richard Wambura ameteuliwa kuwa Kamisaa wa Mchezo Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF CC) kati ya Al Shandy ya Sudan dhidi ya FC Lupopo mchezo utakaochezwa siku ya Jumapili nchini Sudan.
    Refa Israel Nkongo (kulia) atachezesha mechi ya Kombe la Shirikisho

    Mwamuzi Israel Mujuni Nkongo akisaidiwa Frank Komba na Soud Lila, mwamuzi wa akiba akiwa ni Mfaume Ali Nassoro katika mchezo kati ya Renaissance Football Club (Chad) v E.S.T. (Tunisia) wa Kombe la Shirikisho Afrika (CAF CC) nchini Chad.
    Mchezo namba 97 wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika (AFCON) kati ya Lesotho v Shelisheli Machi 29, 2016 utachezeshwa na Israel Mujuni akisaidiwa na Ferdinand Chacha, Samuel Mpenzu huku mwamuzi wa akiba akiwa Waziri Sheha.
    Mwamuzi Mfaume Ali Nassoro atachezesha mchezo kati ya Burundi v Congo DR kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika kwa Vijana wenye umri chini ya miaka 20 (U20), Aprili 4, 2016 mjini Bunjumbura akisaidiwa na Frank John Komba, Alli Kinduli, huku Martin Eliphas Saanya akiwa mwamuzi wa akiba.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAREFA WA BONGO WAPEWA KAZI CAF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top