• HABARI MPYA

    Thursday, March 10, 2016

    KIPA WA SIMBA TAABANI KWA SARATANI YA TUMBO, AMELAZWA ULAYA

    KIPA wa zamani wa Simba ya Tanzania, Abel Dhaira amelazwa hospitali nchini Iceland na hali yake ni mbaya kutokana na ugonjwa wa saratani ya tumbo.
    Dhaira, mwenye umri wa miaka 28, anayechezea klabu ya IBV ya Iceland, amekuwa akilazwa na kuruhusiwa hospitali kwa muda kutokana na saratani ya tumbo ambayo imeathiri maisha yake ya soka.
    Dhaira aliyechezea Simba kwa msimu mmoja wa 2013/2014 kabla ya kurejea Ulaya, kwa sasa ameanza kupatiwa matibabu baada ya klabu yake, IBV Vestmannaeyjar kuanza kuchangisha fedha kwa ajili hiyo.
    Abel Dhaira (kushoto) akiwa hospitali na kulia ni kiongozi wa klabu yake, IBV Vestmannaeyjar

    IBV Vestmannaeyjar imeandaa mchezo wa kirafiki Jumapili kati ya timu ya sasa ya Dhaira na wachezaji wenzake wa zamani dhidi ya timu ya Daraja la Pili.
    Abel Dhaira amecheza kwao Uganda klabu za URA na Express, Tanzania Simba, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) AS Vita na IBV ya Iceland.
    Alianza kuchezea timu ya taifa ya Uganda mwaka 2009 na akacheza Kombe la CECAFA Challenge mwaka 2012, ambako alikimbizwa hospitali na kulazwa baada ya kuzimia kufuatia kugongana na mchezaji mwenzake.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIPA WA SIMBA TAABANI KWA SARATANI YA TUMBO, AMELAZWA ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top