• HABARI MPYA

  Thursday, March 10, 2016

  SIMBA SC KURUDI KILELENI LIGI KUU LEO, AU NDANDA WATAKAZA?

  SIMBA SC ina nafasi ya kurejea kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara leo iwapo itashinda dhidi ya Ndanda FC ya Mtwara.
  Simba wanaikaribisha Ndanda leo katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakihitaji ushindi ili kuongoza ligi.
  Na kocha wa Wekundu hao wa Msimbazi, Mganda Jackson Mayanja amesema kwamba timu yake ipo vizuri baada ya maandalizi ya tangu Jumatatu wakiwa kambini nje kidogo ya mji ili wachezaji wapate utulivu. 
  Simba watarudi kileleni leo mbele ya Ndanda FC?

  “Tunatarajia mchezo mgumu na wenye ushindani mkubwa, lakini tumejiandaa kushinda,”amesema Mayanja.
  Ikumbukwe Simba SC inaongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 48, baada ya kucheza mechi 21, ikiizidi pointi moja Azam FC iliyo nafasi ya tatu na ikizidwa kwa mbili na vinara, Yanga.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC KURUDI KILELENI LIGI KUU LEO, AU NDANDA WATAKAZA? Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top