• HABARI MPYA

  Saturday, March 12, 2016

  JKU 'WAFA KIUME' KAMPALA MBELE YA SC VILLA KOMBE LA SHIRIKISHO

  JKU (pichani juu) ya Zanzibar imefungwa mabao 4-0 katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza Kombe la Shirikisho Afrika Uwanja wa Mandela, Kampala, na wenyeji SC Villa ya Uganda. 
  Mabao ya Jogoo Jogoo la Kampala yamefungwa na Mike Ndera, Mike Serumaga, Umar Kasumba na Godfrey Lwesibawa. Sasa JKU (pichani) itabidi ishinde 5-0 wiki ijayo Uwanja wa Amaan, Zanzibar ili kusonga mbele.
  Wawakilishi wengine wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho, Azam FC wanashuka Uwanja wa Bidvest mjini Johannesbrug, Afrika Kusini kumenyana na wenyeji Bidvest Wits katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza.
  Yanga timu pekee iliyobaki Ligi ya Mabingwa, imeanza vizuri kwa ushindi wa 2-1 ugenini dhdi ya wenyeji APR Uwanja wa Amahoro, Kigali.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JKU 'WAFA KIUME' KAMPALA MBELE YA SC VILLA KOMBE LA SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top