• HABARI MPYA

    Tuesday, March 15, 2016

    AZAM NA YANGA WAONGEZWA VIPORO, SIMBA WATANUNAJE!

    Na Somoe Ng’itu, DAR ES SALAAM
    MECHI mbili za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara zinazozihusu timu za Azam na Yanga zilizopangwa kufanyika mapema wki ijayo, zimeahirishwa.
    Mechi hizo ni kati ya Mtibwa Sugar na Azam FC Jumanne ya Machi 22 Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro na Yanga SC dhidi ya Mwadui FC Jumatano ya Machi 23, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwaka huu.
    Sababu za kufutwa kwa mechi hizo ni kupisha ratiba ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars katika mechi za kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika 2017.
    Kiungo wa Yanga, Deus Kaseke akipasua katikati ya wachezaji wa Azam FC, Serge Wawa (kulia) na Farid Mussa (kushoto)

    taifa Stars itakuwa na mchezo wa kufuzu AFCON Kundi G dhidi ya Chad mjini N’jamena Machi 25, kabla ya timu hizo kurudiana Machi 28, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Na baada ya mechi za mwishoni mwa wiki za michuano ya klabu barani, Afrika wachezaji wa Stars wanatarajiwa kukusanywa Jumapili kabla ya safari Jumanne kuelekea Chad.
    Yanga SC baada ya ushindi wa 2-1 kwenye mchezo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya APR Jumamosi mjini Kigali, watarudiana na timu hiyo ya jeshi la Rwanda Jumamosi wiki hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Na Azam FC baada ya kushinda 3-0 mjini Johannesburg, Afrika Kusini dhidi ya wenyeji Bidvest Wits katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza Kombe la Shirikisho Afrika, watarudiana na timu hiyo Jumapili, Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
    Pamoja na hayo, Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea leo kesho na mwishoni mwa wiki.
    Azam FC wataikaribisha Stand United kesho Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
    Kwa Stand United ikiwa na pointi 30 baada ya kucheza mechi 22 haina nafasi ya ubingwa na wala haimo kwenye hatari ya kushuka daraja, hivyo huo ni mchezo ambao hauwatii ‘presha’ hata kidogo.
    Lakini Azam FC ikiwa nafasi ya tatu kwa pointi zake 47 za mechi 20 katika mbio za ubingwa dhidi ya Yanga yenye pointi 50 za mechi 21 na Simba iliyo kileleni kwa pointi zake 54 za mechi 23 – inahitaji ushindi ili kujiimarisha.  
    Simba itashuka tena dimbani Jumamosi kucheza na Coastal Union Jumamosi Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM NA YANGA WAONGEZWA VIPORO, SIMBA WATANUNAJE! Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top