• HABARI MPYA

  Wednesday, March 16, 2016

  CANNAVARO: MIMI BADO BADO KIDOGO

  Na Renatha Msungu, DAR ES SALAAM
  NAHODHA wa timu ya soka ya Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' amesema kurejea kwake uwanjani kuendelea na kikosi cha wanajangwani hao, kutatokana na ruhusa ya Daktari ambaye anaendelea naye katika mazoezi mepesi, ili kuhakikisha anakuwa fiti.
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE jana, Cannavaro alisema kurejea katika kikosi chake, kutatokana na taarifa ya madaktari kutoka India ambao wanaendelea kumpa mazoezi na matibabu katika kliniki ya Nandal ilioko Msasani jijini Dar es Salaam.
  Nadir Cannavaro (kulia) akiwa na Rais wa zamani wa Tanzania, Dk Jakaya Kikwete (kushoto)

  Cannavaro alisema awali ilipangwa afanyiwe operesheni kwa mara nyingine, lakini baada ya uchunguzi wa madaktari kutoka India, walisema aendelee na  mazoezi mepesi, chini ya uangalizi wa madaktari hao,ambapo atarejea uwanjani wakati wowote watakapomruhusu.
  "Kwa kweli naendelea vizuri, nafanya mazoezi mepesi, kwenye gym,ilio kwenye klini hiyo, chini ya madaktari  jambo ambalo linanipa matumaini ya kurejea uwanjani haraka,"alisema Cannavaro.
  Alisema, ukiacha hilo, pia anafarijika kuona wachezaji wenzake wanapambana uwanjani, ili kuhakikisha Yanga inafanya vizuri katika mechi zake za Ligi Kuu bara na zile za Klabu Bingwa Afrika.
  Alisema kutokana na hilo,amewatoa wasi wasi mashabiki wa Yanga, kuhusiana na yeye kurejea uwanjani, ambapo alisema Daktari akitoa ruhusa, atakuwa tayari kuungana na wenzake katika mechi za Ligi.
  Akizungumzia ushindani kwa ujumla, alisema ligi kwa sasa inaushindani mkubwa, lakini anakiamini kikosi chao, kutokana na uwezo wa kupambana waliokuwa nao uwanjani.
  Cannavaro yuko nje kwa mwezi wa nne sasa, baada ya kupata majeraha akiwa na timu ya taifa wakati wa mechi dhidi ya Algeria iliofanyika Septemba mwaka jana.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CANNAVARO: MIMI BADO BADO KIDOGO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top