• HABARI MPYA

  Wednesday, March 16, 2016

  AZAM VETERANS WACHEZEA 2-1 ZA TABATA

  Mshambuliaji wa Azam Veterans, Salim Aziz 'Riyad Mahrez' kushoto akijaribu kumlamba chenga beki wa Tabata Veterans katika mchezo wa Kundi B michuano ya JMK Floodlight League Uwanja wa kituo cha michezo cha Jakaya Mrisho Kikwete (JKM), KIdongo Chekundu, Dar es Salaam usiku wa Jumanne. Tabata Veterans walishinda 2-1
  Mshambuliaji wa Azam Veterans, Philipo Alando akimtoka beki wa Tabata Veterans
  Mshambuliaji wa Azam Veterans, Abdulkarim Amin 'Popat' akiwapangua mabeki wa Tabata Veterans kabla ya shuti lake kugonga mwamba
  Mfungaji wa bao pekee la Azam Veterans, Mbaraka Shaaban (kulia) akishangilia na Salim Aziz 'Riyad Mahrez' na Philipo Alando (kushoto)
  Kikosi cha Azam Veterans kilichopoteza mechi usiku wa Jumanne
  Mbaraka Shaaban akiambaa na mpira, huku Karim Popat akionekana kujiweka tayari kupokea pasi
  Mkuu wa benchi la Ufundi, Karim Mapesa (wa pili kushoto) akipanga kikosi. Kulia ni kipa wa timu hiyo, Sameer Muchacho ambaye kwa sasa yuko nje kwa maumivu ya bega
  Mchezaji mwingine majeruhi wa Azam Veterans, Omar Ghosh alikuwepo kushuhudia jahazi la timu yake likizama
  Mkuu wa benchi la Ufundi, Karim Mapesa (kulia) akiwa na mchezaji mwingine majeruhi, Jeff Leah (kushoto)
  Kocha Iddi Nassor 'Cheche' akiwapa mipango wachezaji wakati wa mapumziko

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM VETERANS WACHEZEA 2-1 ZA TABATA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top