• HABARI MPYA

  Saturday, March 12, 2016

  AZAM UTAIPENDA, YAWATANDIKA WASAUZI 3-0 KWAO KAMA WAMESIMAMA

  AZAM FC imeanza vyema michuano ya Afrika kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya wenyeji Bidvest Wits jioni ya leo Uwanja wa Bidvest mjini Johannesburg, Afrika Kusini katika mchezo wa kwanza Raundi ya Kwanza Kombe la Shirikisho Afrika.
  Maana yake Azam FC sasa itacheza bila presha mechi ya marudiano Dar es Salaam wiki ijayo, ikihitaji sare kusonga mbele.  
  Mabao ya Azam FC leo yamefungwa na kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’ dakika ya 51, beki Shomary Kapombe dakika ya 56 na mshambuliaji na Nahodha John Bocco ‘Adebayor’ dakika ya 59. 
  Wachezaji wa Azam FC wakimpongeza Nahodha wao, John Bocco (wa pili kulia) baada ya kufunga bao la tatu

  Wawakilishi wengine wa Tanzania, JKU ya Zanzibar wamefungwa mabao 4-0 na wenyeji SC Villa katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza Kombe la Shirikisho Afrika Uwanja wa Mandela, Kampala, Uganda. 
  Mabao ya Jogoo Jogoo la Kampala yamefungwa na Mike Ndera, Mike Serumaga, Umar Kasumba na Godfrey Lwesibawa. Sasa JKU (pichani) itabidi ishinde 5-0 wiki ijayo Uwanja wa Amaan, Zanzibar ili kusonga mbele.
  Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Aishi Manula, Shomari Kapombe/Waziri Salum dk79, Erasto Nyoni, Aggrey Morris, Serge Wawa, Kipre Bolou/Frank Domayo dk83, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Himid Mao, John Bocco ‘Adebayor’, Didier Kavumbagu/Khamis Mcha ‘Vialli’ dk73 na Ramadhani Singano ‘Messi’.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM UTAIPENDA, YAWATANDIKA WASAUZI 3-0 KWAO KAMA WAMESIMAMA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top