• HABARI MPYA

    Sunday, October 04, 2015

    STAND UNITED YAWACHAPA 1-0 MBEYA CITY, PRISONS YAIPIGA 3-0 KAGERA, TOTO YANG’ARA

    MECHI ZIJAZO LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA
    Leo; Okroba 4, 2015
    Toto Africans 1-0 JKT Ruvu
    Stand United 1-0 Mbeya City
    Kagera Sugar 0-3 Prisons
    Oktoba 3, 2015
    Mgambo Shooting 0-0 Coastal 
    Majimaji FC 0-1 Mwadui FC
    MECHI ZIJAZO…  
    Oktoba 17, 2015
    Yang a SC Vs Azam Fc
    Majimaji FC Vs African Sports
    Mbeya City Vs Simba Sc Sokoine
    Ndanda FC Vs Toto Africans
    Stand United Vs Prisons
    Coastal Union Vs Mtibwa Sugar
    Mgambo Shooting Vs Kagera Sugar 
    Mwadui FC Vs JKT Ruvu
    Elias Maguri ameendelea kuifungia mabao Stand United

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    TIMU ya Mbeya City imeendelea kusuasua katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya lao kuchapwa bao 1-0 na Stand United Uwanja wa Kambarage, SHinyanga.
    Shukrani kwake, mfungaji wa bao hilo pekee Elias Maguri dakika ya 47 katika mchezo huo uliokuwa mkali na wa kusisimua.
    JKT Ruvu nayo imeendelea kusuasua baada ya kuchapwa 1-0 na Toto Africans Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza bao pekee la Edward Chiristopher dakika ya 76.
    Kagera Sugar nayo imeendelea kuboronga pia, baada ya kuchapwa 3-0 na Prisons Uwanja wa A.H. Mwinyi, Tabora mabao ya Jeremiah Juma mawili na Ally Manzi moja.
    Mechi za jana, bao pekee la Fabian Gwanse liliipa ushindi wa ugenini wa 1-0 Mwadui FC ya Shinyanga dhidi ya Majimaji Uwanja wa Majimaji, Songea jioni ya leo, wakari Mgambo Shooting ilitoa sare ya bila kufungana Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: STAND UNITED YAWACHAPA 1-0 MBEYA CITY, PRISONS YAIPIGA 3-0 KAGERA, TOTO YANG’ARA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top