• HABARI MPYA

    Sunday, October 25, 2015

    ETHIOPIA NA ZAMBIA ZATINGA CHAN 2016, BURUNDI NA MSUMBIJI ‘ZAANGUKIA PUA’

    TIMU ya Ethiopia imefuzu fainali za Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) 2016 baada ya kuifunga Burundi 3-0 katika mchezo wa marudiano leo mjini Addis Ababa.
    Ethiopia inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-2, baada ya awali kufungwa 2-0 Bujumbura na Burundi, ambayo leo ilimkosa mshambuliaji wake mahiri, Laudit Mavugo aliyekuwa ana kadi mbili za njano. 
    Mavugo ndiye aliyefunga mabao yote ya Burundi katika mchezo wa kwanza. Shujaa wa Walia leo alikuwa Gatoch Panom aliyefunga mabao mawili, wakati bao lingine lilifungwa na Seyoum Tesfaye.
    Ethiopia wakishangilia ushindi wao leo Addis Ababa

    Festus Mbewe alianza kuifungia Chipolopolo leo, kabla ya Momed Hagi kuisawazishia Msumbiji kwa penalti


    Nayo Zambia imefanikiwa pia kufuzu CHAN ya mwakani Rwanda baada ya kuitoa Msumbiji kwa jumla mabao 4-1.
    Chipolopolo waliitandika Mambas 3-0 katika mchezo wa kwanza Uwanja wa Levy Mwanawasa wiki iliyopita mabao ya Winston Kalengo, Conlyde Luchanga na Spencer Sautu kabla ya sare ya 1-1 leo Uwanja wa Machava.
    Festus Mbewe alianza kuifungia Chipolopolo leo dakika ya 20 kabla ya Momed Hagi kuisawazishia Msumbiji dakika ya 85 kwa penalti, kufuatia Christopher Munthali kuunawa mpira.
    Zambia sasa inaungana na wenyeji Rwanda), Angola, Gabon, Guinea, Mali, DR Congo, Morocco, Ethiopia na Tunisia ambazo tayari zimefuzu.
    Ratiba ya fainali hizo inatarajiwa kupangwa Kigali Novemba 18, mwaka huu na Rwanda itakuwa mwenyeji wa CHAN ya nne tangu kuanzihwa michuano hiyo inayoshirikisha wachezaji wanaocbeza ligi za nchini mwao pekee.
    CHAN inatarajiwa kuanza Januari 16 hadi Februari 7 mwakani.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ETHIOPIA NA ZAMBIA ZATINGA CHAN 2016, BURUNDI NA MSUMBIJI ‘ZAANGUKIA PUA’ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top