• HABARI MPYA

    Tuesday, October 27, 2015

    KOCHA MJERUMANI WA TOTO ABWAGA MANYANGA KISA WACHGEZAJI HAWALIPWI MISHAHARA, MAZOEZI YA ‘KUUNGA UNGA’

    RATIBA LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA WIKI HII
    Oktoba 28, 2015
    Toto African Vs Mgambo Shooting
    Mwadui FC Vs Yanga SC
    Mtibwa Sugar Vs Kagera Sugar
    Mbeya City Vs Majimaji Fc Sokoine
    Ndanda FC Vs Stand United
    Simba Sc Vs Coastal Union
    Oktoba 29, 2015
    JKT Ruvu Vs Azam FC 
    Prisons Vs African Sports
    Kocha wa Toto, Martin Grelis (katikati) akiwa na Wasaidizi wake hivi karibuni

    Na Alex Sanga, MWANZA

    KOCHA Mjerumani wa Toto Africans ya Mwanza, Martin Grelis ameachia ngazi katika timu hiyo, akitoa sababu zaidi ya tatu, kubwa ni wachezaji kutothaminiwa na uongozi mbovu wa timu.
    Katika barua yake ambayo BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE imefanikiwa kupata nakala yake, Grelis aliyeanza kazi Julai mwaka huu, amesema kwamba ameamua kuacha kazi baada ya kugundua hata wachezaji hawalipwi mishahara.
    Aidha, safari za ‘kigumu’ kwenda mikoa ya Tanga na Tabora katika mechi zao za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara nazo zimechangia kumfanya aachie ngazi, ingawa mwenendo wa timu si mbaya hadi sasa.
    “Kwa mwezi mzima tumefanya mazoezi ya uhakika mara saba tu, hali ambayo kocha yeyote hawezi kukubaliana nayo, nami kama kocha, imenilazimu kuchukua uamuzi huu ambao ungechukuliwa na kocha yeyote,”amesema.
    Aidha, Grelis amesema kwamba wachezaji kutothaminiwa na kwa ujumla uongozi mbovu wa timu, navyo vimemfanya ashindwe kabisa kuendelea na kazi katika timu hiyo ya Mtaa wa Kishamapanda, Mwanza.
    Hata hivyo, Grelis amesema anaamini kujiuzulu kwake kutaufanya uongozi ubadilike na kurekebisha mwenendo wake ndani ya timu, akiamini Toto ina wachezaji wazuri watakaoifanya timu iwe imara.
    “Naamini, Toto ni timu yenye wachezaji wazuri, ambao wataifanya timu iweze kushindana na timu bora na kudumu katika Ligi Kuu. Itakuwa majanga sana iwapo, uongozi utashindwa kuwatimizia wachezaji mahitaji yao, ili waweze kucheza vizuri,”amesema.
    Grelis anaiacha Toto ikiwa katika nafasi ya tisa kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kuvuna pointi 10 katika mechi nane. 
    Hii ni nakala ya barua yake ya kujiuzulu

    Mara ya mwisho, Grelis alikuwa kwenye benchi la Toto ikifungwa mabao 4-1 na Yanga SC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na amesema matokeo hayio hayahusiani na kujiuzulu kwake.
    Toto inatarajiwa kushuka tena dimbani kesho, Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza kumenyana na Mgambo Shooting ya Tanga katika mfululizo wa ligi hiyo. 
    Kwa ujumla, Ligi Kuu inaendelea kesho, mbali na Toto na Mgambo- pia Mwadui FC watakuwa wenyeji wa Yanga SC Uwanja wa Kambarage Shinyanga, Simba watakuwa wenyeji wa Coastal Union Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Mtibwa Sugar watakuwa wenyeji wa ndugu zao Kagera Sugar Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro.
    Mechi nyingine, Mbeya City watakuwa wenyeji wa Majimaji FC Uwanja wa Sokoine, Ndanda FC wataikaribisha Stand United Uwanja wa Nangwanda, Mtwara wakati keshokutwa JKT Ruvu watamenyana na Azam FC Uwanja wa Karume, Dar es Salaam na Prisons wataikaribisha African Sports Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
    Grelis akiwa na wachezaji wa Toto mazoezini Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KOCHA MJERUMANI WA TOTO ABWAGA MANYANGA KISA WACHGEZAJI HAWALIPWI MISHAHARA, MAZOEZI YA ‘KUUNGA UNGA’ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top