• HABARI MPYA

    Friday, October 30, 2015

    MALINZI AMPA NENO MAGUFULI MAPEMA KUHUSU MICHEZO TANZANIA

    RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemtumia salamu za pongezi Dk. John Pombe Joseph Magufuli kufuatia kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
    Katika salamu zake, Malinzi amesema TFF ina imani na ahadi za mikakati yake ya kuongeza uwekezaji wa Serikali katika maendeleo ya mpira wa miguu na michezo kwa ujumla.
    Jana, Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania (NEC) ilitangaza Rais mpya na awa mua ya tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kumshinda mpinzani wake mkuu, Edward Ngoyai Lowassa wa CHADEMA na UKAWA.
    Dk Magufuli akiwa na Rais aliyemaliza muda wake, Dk Jakaya Kikwete

    Akitangaza matokeo rasmi ya uchaguzi wa rais, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, (NEC) Jaji Mstaafu Damian Lubuva alisema Dk Magufuli amepata kura 8, 882, 935, wakati Lowassa amepata kura 6, 072, 848.
    Kwa mujibu wa Jaji Lubuva idadi ya wapiga kura ilikuwa 15, 589,639 sawa na asimilia 67.1 ambapo kura halali zilikuwa 15,193,862 sawa asilimia 97.46.
    Aidha amesema idadi ya waliojiandikisha kupiga kura nchi nzima ni 23,161, 440. Amesema vyama sita vimetia saini kukubali matokea hayo kati vyama vinane vilivyoshiriki uchaguzi huo wa rais.
    Magufuli anakuwa Rais  wa tatu ndani ya mfumo wa Vyama Vingi vya Siasa nchini, baada ya Benjamin William Mkapa (1995-2005) na Jakaya Mrisho Kikwete (2005-2015) wote wa CCM na Rais wa tano jumla wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, (1961-1985) na Ally Hassan Mwinyi (1985-1995) waliowatangulia Mkapa na Kikwete.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MALINZI AMPA NENO MAGUFULI MAPEMA KUHUSU MICHEZO TANZANIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top