• HABARI MPYA

    Saturday, October 17, 2015

    DIWANI MTARAJIWA SAID FELA AWAFARIJI WAGONJWA HOSPITALI MBAGALA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    TAASISI ya Mkubwa na Wanawe inayomilikiwa na Mkurugenzi wake Said Fella 'Mkubwa Fella' jana ilitembelea Wodi ya Wanawake na Watoto katika Hospital ya Mbagala Zakhem Jijini Dar es Salaam.
    Akizungumza na waandishi wa habari Hospitalini hapo ambapo alikuja kutoa vifaa mbalimbali kwa wagonjwa sambamba nakufanya usafiki katika eneo la hospitali hiyo.
    Fella alisema, ameguswa kuitembelea hospitali hiyo na ataendelea kufanya hivyo kupitia umoja wa vikundi vya Joging saba alivyoviunda katika kata yake ya Kilungule anakowania Udiwani.
    Said Fela (kushoto) akikabidhi misaada kwa Daktari wa hospitali ya Mbagala Zakhem, Dar es Salaam, Adam Silas (kushoto)
    Fela akiwa amembeba mmoja wa watoto waliozaliwa nje ya wadi ya Wazazi hospitalini hapo
    Fela akimpa zawadi mtoto aliyezaliwa katika wadi ya Wazazi



    "Tumekuja hapa Hospitali kuwasalimia wagonjwa na tumewaletea kitu kidogo tulichojaaliwa kama unavyoona Sabun, dawa za meno, soda, juice na vitu mbalimbali,"alisema Fella.
    Akizungumzia msaada huo Dk Silas Adam alimshukuru Fella kwa sapoti yake na kuona umuhimu wa kuwatembelea wanawake na watoto katika Hospitali hiyo.
    Silas alisema, licha ya shukurani hiyo ya vifaa hivyo amemuomba Fella kuwasaidia damu kupitia vijana wake hao kwani wanachangamoto kubwa ya damu hasa katika wodi ya wazazi.
    "Tunamshukuru sana Fella kwa kidogo alichojaliwa kukileta kwetu ni faraja kubwa sana kwetu, tunatambua alivyotoa mchango mkubwa kwa vijana hapa nchini. hivyo basi kupitia vijana wake hao tunakuomba utusaidie waje watoe damu,"alisema.
    Aliongeza kwa kuwataka Watanzania wengine kuwa na moyo kama wa Fella kusaidia watu mbalimbali hata kama sio katika hospitali hiyo.
    Naye Mwenyekiti wa umoja wa vikundi hivyo vya jogging  Salimu Omary alisema wametembelea hospitali hiyo ikiwa ni siku moja kabla ya kuzindua umoja wao kupitia kata ya Kilungule ambapo uzinduzi huo unafayika leo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DIWANI MTARAJIWA SAID FELA AWAFARIJI WAGONJWA HOSPITALI MBAGALA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top