• HABARI MPYA

    Wednesday, October 21, 2015

    PRISONS WAISWEKA ‘LUPANGO SIMBA SC, WAITANDIKA 1-0, NGONGOTI WA SENEGAL ADAIWA KUCHEZA NA 'KITU' SOKOINE

    Na Princess Asia, MBEYA
    BAO pekee la Mohammed Mkopi dakika ya 62 limeipa Prisons FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Simba SC jioni ya leo Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    Hicho kinakuwa kipigo cha pili kwa Simba SC inayofundishwa na Muingereza Dylan Kerr katika Ligi Kuu msimu huu, baada ya awali kufungwa 2-0 na mahasimu, Yanga SC. 
    Mchezo huo ulisimama kwa dakika nne kipindi cha kwanza, baada ya Nahodha wa Prisons, kudai mchezaji wa Simba SC, Pape Ndaw, ana kitu mfano wa hirizi kiunoni.
    Mshambuliaji Msenegali wa Simba SC, Pape Ndaw akitafuta maarifa ya kumtoka beki wa Prisons, Laurian Mpalile
    Jumanne Elfadhil wa Prisons akimtoka Mohammed Hussein 'Tshabalala' wa Simba SC

    Suala hilo lilifika kwa mwamuzi na mchezaji huyo kupelekwa katika chumba maalum na kukaguliwa na msimamizi wa mechi hiyo, Joseph Mapunda.
    Hata hivyo, zilitokea vurugu za hapa na pale kwa kila upande ukiona unaonewa, ingawa Ndaw alirejea uwanjani kuendelea na mchezo baada ya ukaguzi huo. 
    Katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu leo, mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Elias Maguri amefunga mabao mawili dakika za 47 na 60 timu yake, Stand United ikishinda 3-0 dhidi ya Majimaji ya Songea Uwanja wa Kambarage Shinyanga, bao lingine likifungwa na Pastory Athanas dakika ya 66.
    Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Vincent Angban, Hassan Kessy, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Hassan Isihaka, Juuko Murshid, Justice Majabvi,  Simon Sserunkuma/Mwinyi Kazimoto, Awadh Juma/Said Ndemla, Pape Ndaw, Joseph Kimwaga na Peter Mwalyazi/Ibrahim Hajib.
    Prisons; Aron Kalambo, Laurian Mpalile/Beno Kakolanya, Salum Kimenya, Nurdin Chona, James Mwasote, Jumanne Elfadhili, Lambart Sabiyanka, Juma Seif ‘Kijiko’/Ally Milanzi, Mohammed Mkopi, Jeremiah Juma na Benjamin Asukile.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PRISONS WAISWEKA ‘LUPANGO SIMBA SC, WAITANDIKA 1-0, NGONGOTI WA SENEGAL ADAIWA KUCHEZA NA 'KITU' SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top