• HABARI MPYA

    Monday, October 26, 2015

    ZAMBIA WAOMBA KUCHEZA CHALLENGE, CECAFA 'YAWALETEA MAPOZI'

    BARAZA la Soka la Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limepokea maombi kutoka Zambia na Malawi wakitaka timu zao za taifa (Chipolopolo, The Flames) zishiriki Kombe la Challenge mwaka huu.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE kwa simu jana kutoka Nairobi, Kenya, Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholas Musonye, alisema kwamba Sekretarieti yake itajadili maombi hayo pamoja na wenyeji Ethiopia.
    Musonye alisema kuwa maandalizi mengine ya michuano hiyo inatarajiwa kuanza Novemba 21 hadi Desemba 6 mwaka huu Addis Ababa, yako katika hatua za mwisho na wanatarajia mashindano ya mwaka huu yatakuwa na changamoto zinazotokana na wawakilishi kujiandaa na fainali za mwakani za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN).
    Kikosi cha Malawi kilichoomba kucheza michuano ya Challenge mwaka huu Ethiopia

    Alisema kuwa nchi pekee mwanachama ambayo haijathibitisha kushiriki michuano hiyo hadi jana ni Eritrea ambayo pia mwaka juzi haikushiriki.
    Mwaka jana mashindano hayo hayakufanyika kutokana na Ethiopia ambayo ilithibitisha kuwa mwenyeji kujiondoa katika dakika za meishoni na CECAFA kukosa mwenyeji mbadala.
    Harambee Stars ya Kenya iliyokuwa inasheherekea miaka 50 ya Uhuru wa nchi yao ndiyo mabingwa watetezi wa mashindano hayo baada ya kuwafunga Sudan mabao 2-0 katika mechi ya fainali iliyofanyika kwenye Uwanja wa Nyayo jijini Nairobi huku.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ZAMBIA WAOMBA KUCHEZA CHALLENGE, CECAFA 'YAWALETEA MAPOZI' Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top