• HABARI MPYA

    Saturday, October 17, 2015

    YANGA YAWAANZISHA BUSUNGU, TAMBWE NA NGOMA… HUKO AZAM SASA BALAA, WANGA NA BOCCO WAANZISHWA WOTE MBELE

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    KOCHA Mholanzi wa Yanga SC, Hans van der Pluijm amewaanzisha pamoja washambuliaji Mrundi, Amisi Tambwe, Mzimbabwe Donald Ngoma na mzalendo Malimi Busungu katika mchezo dhidi ya Azam FC jioni ya leo.
    Yanga SC inamenyana na Azam FC kuanzia Saa 10:00 jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    Na Pluijm amemchezesha Mbuyu Twite katika nafasi ya kiungo wa ulinzi, pamoja na Salum Telela, wakati kiungo mchezeshaji hii leo ni Thabani Kamusoko.
    Safu ya ulinzi ya Yanga SC inaundwa na kipa Ally Mustafa ‘Barthez’, beki wa kulia Juma Abdul, kushoto Mwinyi Mngwali na katikati Kevin Yondan na Nadir Haroub ‘Cannavaro’. 
    Picha linajirudia; Farid Mussa atakutana tena na Juma Abdul leo

    Katika benchi wapo Deo Munishi ‘Dida’, Vincent Bossou, Said Juma ‘Makapu’, Deus Kaseke, Simon Msuva, Andrey Coutinho na Matheo Anthony.
    Upande wa Azam FC, kocha Muingereza Stewart John Hall amewaanzisha pamoja washambuliaji wawili wenye nguvu na miili mikubwa, Mkenya Alan Wanga na mzalendo John Bocco. 
    Vikosi vinqvyoanza leo ni;
    Yanga SC, Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Mwinyi Mngwali, Kevin Yondan, Nadir Cannavaro, Mbuyu Twite, Salum Telela, Thabani Kamusoko, Donald Ngoma, Amissi Tambwe na Malimi Busungu.  
    Benchi; Deo Munishi ‘Dida’, Vincent Bossou, Said Juma ‘Makapu’, Deus Kaseke, Simon Msuva, Andrey Coutinho na Matheo Anthony.
    Azam FC; Aishi Manula, Aggrey Morris, David Mwantika, Serge Wawa Pascal, Shomary Kapombe, Farid Mussa Shah Malik, Kipre Balou, Himidi Mao, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Allan Wanga na John Bocco.
    Benchi; Mwadini Ali, Kipre Tchetche, Ramadhani Singano ‘Messi’, Frank Domayo, Said Mourad, Erasto Nyoni na Mudathir Yahya.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA YAWAANZISHA BUSUNGU, TAMBWE NA NGOMA… HUKO AZAM SASA BALAA, WANGA NA BOCCO WAANZISHWA WOTE MBELE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top