• HABARI MPYA

    Sunday, October 04, 2015

    SANCHEZ APIGA MBILI ARSENAL YAIFUMUA 3-0 MAN UNITED, LIVERPOOL 1-1 NA EVERTON

    ARSENAL imetumia vizuri fursa ya kucheza mbele ya umati wa mashabiki wake Uwanja wa Emirates kwa kuifunga mabao 3-0 Manchester United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni ya leo. 
    Alexis Sanchez alifunga mabao mawili katika ushindi huo, la kwanza dakika ya sita na la tatu dakika ya 19, wakati bao la pili limefungwa na Mesut Ozil dakika ya saba.
    Hii ni mara ya kwanza United kufungwa mabao matatu ndani ya dakika 20 katika mechi ya Ligi Kuu ya England.
    Kikosi cha Arsenal kilikuwa; Cech, Bellerin, Mertesacker, Gabriel, Monreal, Coquelin, Cazorla, Ramsey, Ozil/Oxlade-Chamberlain dk75, Sanchez/Gibbs dk81 na Walcott/Giroud dk75.
    Manchester United; De Gea, Darmian/Valencia dk46, Smalling, Blind, Young, Carrick, Schweinsteiger, Mata/Wilson dk82, Rooney, Depay/Fellaini dk46 na Martial.
    Katika michezo mingine ya ligi hiyo leo, Everton imelazimishwa sare ya 1-1 na Liverpool Uwanja wa Goodison Park. Danny Ings alianza kuwafungia wageni dakika ya 41, kabla ya Romelu Lukaku kusawazisha dakika ya 45 na ushei.
    Mshambuliaji Alexis Sanchez akiteleza chini kushangilia mbele ya mashabiki wa Arsenal PICHA ZAIDI GONGA HAPA
    Danny Ings (katikati kushoto) akipiga kichwa kuifungia Liverpool bao la kuongoza dhidi ya Everton PICHA ZAIDI GONGA HAPA
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SANCHEZ APIGA MBILI ARSENAL YAIFUMUA 3-0 MAN UNITED, LIVERPOOL 1-1 NA EVERTON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top