• HABARI MPYA

    Tuesday, October 20, 2015

    MECHI YA SIMBA NA AZAM YAAHIRISHWA KUPISHA MAANDALIZI YA STARS NA ALGERIA

    MECHI za raundi ya 11 za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara zilizokuwa zichezwe Novemba 7 na 8 mwaka huu sasa zitafanyika Desemba 12 na 13 kupisha maandalizi ya Taifa Stars ya mechi za mchujo za Kombe la Dunia.
    Taifa Stars inatarajia kuingia kambini mapema mwezi ujao kujiandaa na mechi ya kwanza dhidi ya Algeria ambayo itafanyika Novemba 14 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Timu hizo zitarudiana nchini Algeria, Novemba 17 mwaka huu.

    Mshambuliaji wa Azam FC, Kipre Tchetche akimtoka beki Mohammed Hussein 'Tshabalala' wa Simba SC katika mechi ya msimu uliopita baina ya timu hizo 

    Mechi hizo za Vodacom zitakazochezwa Desemba 12 ni kati ya Mgambo Shooting na Yanga (Tanga), Kagera Sugar na Ndanda (Tabora), Stand United na Mwadui (Shinyanga), Mbeya City na Mtibwa Sugar (Mbeya), Azam na Simba (Dar es Salaam) na Majimaji na Toto Africans (Songea). Mechi za Desemba 13 ni kati ya JKT Ruvu na Tanzania Prisons (Dar es Salaam), na Coastal Union na African Sports (Tanga).
    Pia mechi tatu za raundi ya sita ambazo hazikuchezwa Oktoba 4 mwaka huu kupisha mechi ya Taifa Stars na Malawi sasa zitafanyika Desemba 16 mwaka huu. Mechi hizo ni kati ya Azam na Mtibwa Sugar (Dar es Salaam), na African Sports na Yanga (Tanga), mchezo kati ya Ndanda na Simba (Mtwara utapangiwa tarehe ya kuchezwa.
    Nayo mechi namba 59 kati ya JKT Ruvu na Mtibwa Sugar iliyokuwa ichezwe Oktoba 21 mwaka huu Uwanja wa Karume, Dar es Salaam imesogezwa mbele kwa siku moja hadi Oktoba 22 mwaka huu ili kuipa nafasi ya mapumziko JKT Ruvu ambayo jana (Oktoba 18 mwaka huu) ilicheza mechi yake ya raundi saba mkoani Shinyanga.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MECHI YA SIMBA NA AZAM YAAHIRISHWA KUPISHA MAANDALIZI YA STARS NA ALGERIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top