• HABARI MPYA

    Sunday, October 04, 2015

    BRENDAN RODGERS 'ATUPIWA VIRAGO' LIVERPOOL, APEWA TAARIFA KWA SIMU

    KOCHA Brendan Rodgers amefukuzwa kazi Liverpool usiku huu kufuatia matokeo mabaya katika Ligi Kuu ya England.
    Raia huyo wa Ireland Kaskazini aliambiwa baada ya sare ya 1-1 na Everton leo kwamba miaka yake mitatu na nusu ya kuanya kazi Anfield imetosha.
    Rodgers, ambaye timu yake imeshinda mechi moja tu kati ya tisa zilizopita ndani ya dakika 90, amepewa taarifa hizo kwa simu juu ya kufukuzwa kwake.   
    Rodgers amekuwa kocha wa Wekundu hao tangu Juni mwaka 2012 alipotua akitokea Swansea City na alisaini Mkataba mpya wa miaka minne zaidi ya mwaka mmoja uliopita.
    Liverpool imeachana na kocha Brendan Rodgers baada ya mwanzo mbaya msimu huu
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BRENDAN RODGERS 'ATUPIWA VIRAGO' LIVERPOOL, APEWA TAARIFA KWA SIMU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top