• HABARI MPYA

    Monday, October 05, 2015

    NI ETOILE NA ORLANDO PIRATES FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA, AL AHLY YAVULIWA TAJI

    RATIBA YA FAINALI MICHUANO YA AFRIKA
    Ligi ya Mabingwa
    Jumapili Novemba 1, 2015
    USM Alger (Algeria) v TP Mazembe (DRC)
    Jumapili Novemba 8, 2015

    TP Mazembe (DRC) v USM Alger (Algeria)
    Kombe la Shirikisho
    Ijumaa Novemba 20, 2015
    Orlando Pirates (Afrika Kusini) v ES Sahel (Tunisia)
    Jumapili Novemba 29, 2015
    ES Sahel (Tunisia) v Orlando Pirates (Afrika Kusini) 

    FAINALI ya Kombe la Shirikisho Afrika mwaka huu, itazikutanisha Etoile du Sahel ya Tunisia na Orlando Pirates ya Afrika Kusini.
    Hiyo inafuatia Pirates kuwatoa waliokuwa mabingwa watetezi, Al Ahly ya Misri jana kwa jumla ya mabao 5-3.
    Pirates imeifunga mabao 4-3 usiku wa jana Al Ahly Uwanja wa Jeshi wa Suez nchini Misri, baada ya awali kushinda 1-0 nyumbani.
    Etoile ilitangulia Fainali juzi licha ya kufungwa mabao 3-0 na wenyeji Zamalek Uwanja wa Petro Sport mjini Cairo, Misri.
    Etoile imefuzu kwa ushindi wa jumla wa 5-4, baada ya awali kuibuka na ushindi wa 5-1 nyumbani, Uwanja wa Olimpiki mjini Sousse, Tunisia.
    Etoile iliyoitoa Yanga SC katika hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo, juzi ilishindwa kuutumia mwanya wa Zamalek kucheza pungufu ya mchezaji mmoja tangu dakika ya tano baada ya mchezaji wake, Ali Gabr kutolewa kwa kadi nyekundu kwa kumpiga usoni Baghdad Bounedjah.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NI ETOILE NA ORLANDO PIRATES FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA, AL AHLY YAVULIWA TAJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top