• HABARI MPYA

    Monday, October 05, 2015

    WASOMALI KUCHEZESHA TAIFA STARS NA MALAWI JUMATANO TAIFA, HICHO KIINGILIO SASA USHINDWE MWENYEWE!

    MAREFA wa mchezo wa kwanza wa kufuzu Kombe la Dunia kati ya wenyeji Tanzania na Malawi keshokutwa wanatoka Somalia na wanatarajiwa kuwasili leo nchini na kufikia katika hoteli ya Protea iliyopo Oysterbay, Dar es Salaam.
    Refa wa kati ni Hagi Yabarow Wiish atakayesaidiwa na Hamza Hagi Abdi, Salah Omar Abubakar, wakati mezani atakuwa Bashir Olad Arab wote wa Waomali na mtathmini wa waamuzi ni Sam Essam Islam wa Misri.
    Kamisaa wa mchezo ni Muzambi Gladmore (Zimbabwe) na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza viingilio vya mchezo, kiingilio nafuu zaidi kikiwa ni Shilingi 5,000.

    Kiingilio cha juu kabisa kwa mchezo huo Shilingi 10,000 kwa viti vya VIP B na C, huku viti vya rangi ya chungwa, bluu na kijani ikiwa ni shilingi elfu tano 5,000.
    Stars inayonolewa na kocha mzawa Charles Boniface Mkwasa imeendelea kujifua katika viwanja vya Gymkhana na uwanja Taifa jioni kujiandaa mchezo huo wa Jumatano dhidi ya Malawi, huku wachezaji wakiwa wenye ari na morali ya hali ya juu kuelekea kwenye mechi hiyo.
    Wachezaji 22 wapo kambini akiwemo mshambuliaji Mrisho Ngasa anayecheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini aliyeripoti jana mchana kambini, huku wachezaji wawili Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wakitarajiwa kujiunga na wenzao leo wakitokea Lubumbashi, DRC.
    Wakati huo huo timu ya Taifa ya Malawi (The Flames) imewasili nchini jana saa 4 asubuhi na kufikia katika hoteli ya De Mag iliyopo Mwanayamala, ambapo kikosi hicho leo kimefanya mazoezi asubuhi katika uwanja wa Boko Veterani.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WASOMALI KUCHEZESHA TAIFA STARS NA MALAWI JUMATANO TAIFA, HICHO KIINGILIO SASA USHINDWE MWENYEWE! Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top