• HABARI MPYA

    Sunday, October 04, 2015

    SAMATA AIPELEKA MAZEMBE FAINALI LIGI YA MABINGWA, APIGA MBILI MERREIKH YAFA 3-0

    SAMATA, SAMATA, SAMATAAAA. Uwanja mzima Samatta. Lubumbashi yote Samata. Mashabiki leo wameimba jina Samata Uwanja wa Mazembe, kufuatia mshambuliaji Mbwana Ally Samata kufunga mabao mawili katika ushindi wa 3-0 dhidi ya El Merreikh ya Sudan.
    Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Tanzania, amefunga mabao hayo katika mchezo wa marudiano wa Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kuiwezesha TP Mazembe kwenda fainali ya michuano hiyo kwa mara ya kwanza baada ya miaka mitano.
    Mbwana Samatta amekuwa shujaa wa Mazembe leo ikikata tiketi ya Fainali Ligi ya Mabingwa Afrika 

    Nyota wa zamani wa Simba SC ya Dar es Salaam, Samatta alifunga bao la kwanza dakika ya 53, akimalizia pasi ya Adama Traore kabla ya kufunga la pili dakika ya 69 kwa pasi ya Yaw Frimpong.
    Mshambuliaji mwingine wa Tanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Rainford Kalaba alishiriki bao la tatu lililofungwa na Roger Assale dakika ya 71.
    Mazembe inayosonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 4-2 baada ya awali kufungwa 2-1 Khartoum, sasa itakutana na USM Alger iliyoitoa El HIlal ya Sudan katika fainali ya Ligi ya Mabingwa AFrika mwaka huu.
    Kikosi cha Mazembe kilikuwa; R. Kidiaba/T. Ulimwengu dk58, J. Kasusula, Y. Frimpong, J. Kimwaki, S. Coulibaly, Asante/R. Assale dk46, B. Diarra, D. Adjei Nii/ M. Bokadi dk85, R. Kalaba, M. Samatta na A. Traore.
    El Merreikh; J. Salim, Ala'a Eldin Yousif, Musaab Omer, Ayman Saied, Ragei Abdallah, Amir Kamal, Ramadan Agab, D. Libere/Ahmed Abdalla dk68, Bakri Al Madina, S. Jabason na F. Coffie/Omar Bakheet dk69.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SAMATA AIPELEKA MAZEMBE FAINALI LIGI YA MABINGWA, APIGA MBILI MERREIKH YAFA 3-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top