• HABARI MPYA

  Monday, February 11, 2019

  MIKE TYSON AVUTA MSOKOTO MKUBWA WA BANGI HADHARANI

  BAADA ya kutamba katika ulimwengu wa ngumi, sasa Mike Tyson ameamua kuzeeka vibaya akiwa katika miaka yake ya 50.
  Bingwa huyo wa zamani wa dunia amekuwa akivuta msokoto mkubwa mno kwenye tamasha maalum la kuvuta bangi, sasa akitoka kuwa 'Mtu Mbaya Duniani' hadi kuwa 'Mtu Mkubwa Zaidi Duniani.'
  Si hivyo tu kwa Iron Mike, kwani Tyson anamiliki ekari 40 za shamba halali la bangi karibu na California, Death Valley, ambalo alilianzisha baada ya Serikali ya Marekani kuhalalisha dawa hizo za kulevya.

  Mike Tyson akivuta msokoto mkubwa kwenye tamasha maalum la kuvuta bangi

  Tyson pia alikiri kuvuta bangi kabla ya pambano lake na Andrew Golota mwaka 2000, ambalo alishinda baada ya Golota kutorejea kuendelea na pambano Raundi ya tatu. 
  Tyson alishinda kwa Technical Knockout (TKO), lakini akapokonywa ushindi wake baada ya vipimo kuonyesha alivuta bangi kabla ya pambano na matokeo yakafutwa. 
  Alisema amekuwa akivuta bangi katika maisha yake yote, lakini akadai ni katika pambano dhidi ya Golota tu ndiyo alipanda ulingoni amevuta dawa hizo, na akasema; "Haikunidhuru mimi, ilimdhuru Golota.' 
  Tyson ni muumini mkubwa wa uvutaji bangi, kwani pia ana shule yake maalum ya kufundisha wakulima wanaochipukia wa bangi iitwayo 'The Tyson Cultivation School.' 
  Pia anataka kupiga hatua zaidi kwa kufanya utafiti wa faida za bangi, hususan CBD, ambayo haina psychoactive na hutumika kutibu magonjwa ya kudhoofu kwa mwili. 
  Pia inatarajiwa kuwa biashara ya faida kwa Tyson, ambayo mauzo ya bangi halali yanakadiriwa kufika dola za Kimarekani Bilioni 24.5 hadi mwaka 2021, kwa mujibu wa jarida la utafiti la Forbes. 
  Na Tyson hakuonekana kuwa mwenye maumivu yoyote kuvuta bangi kubwa hadharani kwenye tamasha hilo akiwa ana umri wa miaka 52.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MIKE TYSON AVUTA MSOKOTO MKUBWA WA BANGI HADHARANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top