• HABARI MPYA

  Sunday, April 08, 2018

  TWIGA STARS YATUPWA NJE KWA MABAO YA UGENINI FAINALI WANAWAKE 2018

  TIMU ya soka ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania, Twiga Stars imetupwa nje ya mbio za kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AWC) Novemba mwaka huu nchini Ghana baada ya sare ya 1-1 na wenyeji Zambia leo.
  Sare hiyo inafanya matokeo ya jumla yawe sare ya 4-4 baada ya timu hizo kufungana mabao 3-3 katika mchezo wa kwanza Dar es Salaam Jumatano wiki hii Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam na sasa Shepolopolo wanasonga mbele kwa faida ya mabao ya ugenini.
  Shepolopolo walitangulia kwa bao la dakika ya kwanza ya Rachel Kundananji, kabla ya Mwanahamisi Omar 'Gaucho' kuisawazishia Twiga Stars dakika ya 72.
  Shepolopolo sasa itakutana na jirani zao wengine, Zimbabwe katika raundi ya mwisho ya mchujo mwezi Juni baada ya wenzao hao kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 4-0 ikishinda 2-0 nyumbani dhidi ya Namibia leo, baada ya kushinda pia 2-0 ugenini kwenye mechi ya kwanza.
  Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake zinatarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu jijini Accra, Ghana wakati zile za dunia zitafanyika mwakani Paris, Ufaransa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TWIGA STARS YATUPWA NJE KWA MABAO YA UGENINI FAINALI WANAWAKE 2018 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top