• HABARI MPYA

    Thursday, April 05, 2018

    TUKUYU STARS KUSHIRIKI LIGI YA MABINGWA WA MIKOA 2018

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MABINGWA wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara mwaka 1986, Tukutu Stars ni miongoni mwa timu 28 zinazotarajiwa kushiriki Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) msimu wa 2017/18 inayotarajiwa kuanza Mei 1 16, mwaka 2018 kwenye vituo vine ambayo ni Geita, Singida, Rukwa na Kilimanjaro. 
    Taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imesema kwamba kila kundi litakuwa na timu saba na timu zitapangwa kwenye vituo vilivyopo ndani ya kanda yake.
    TFF imesema kwamba mwisho wa kuwasilisha jina la bingwa wa mkoa ilikua Machi 30, mwaka huu na mikoa yote 26 iliweza kuwasilisha jina la bingwa wake ndani ya muda.
    Kikosi cha Tukuyu Stars ya Mbeya mwaka 1992 kutoka kushoto Mohamed Kassanda, Suleiman Mrisho, Assanga Aswile, Issah Mohamed, Pio Mwashitete, Jabir Mohamed ‘Jeby’ na Gamshad Gaudast. Waliochuchumaa ni Kanza Mrisho, Raphael Mapunda, Ikupilika Nkoba, Juma Ahmad, Chachala Muya, Robson, Daudi Kufakunoga na Michael Kidilu.

    Timu zinazotarajiwa kucheza ligi hiyo msimu huu Karume Market, Ungindoni FC na Temeke Squad za Dar es Salaam Stand FC ya Pwani, Moro Kids ya Morogoro, Gwassa Sports Club ya Dodoma, Stand Dortmund ya Singida, Tabora FC ya Tabora, Red Stars FC ya Kigoma, Gipco FC ya Geita na Kamunyange FC ya Kagera.
    Nyingine ni Fathom SC ya Mwanza, Nyamongo SC ya Mara, Zimamoto FC ya Shinyanga, Ambassador FC ya Simiyu, Bishoo Durning Sports ya Arusha, Usalama SC ya Manyara, Uzunguni FC ya Kilimanjaro, Sahare All Stars ya Tanga, Maji Maji Rangers ya Lindi, Mwena FC ya Mtwara, Black Belt ya Ruvuma, Kipagalo FC ya Njombe, Migombani FC ya Songwe, Tukuyu Stars ya Mbeya, Iringa United ya Iringa, Laela FC ya Rukwa na Watu FC ya Katavi.
    TFF imesema wawakilishi wa mikoa ya Rukwa, Ruvuma na Tabora hawajatajwa katika orodha hiyo kutokana na malalamiko ya klabu kupinga mabingwa wa mikoa hiyo, ambayo yanayafanyiwa kazi kwa sasa.
    Kundi A litakalokuwa Geita litaundwa na timu za mikoa ya Geita yenyewe, Kagera, Mara, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Dar es Salaam, wakati Kundi B litakalokuwa Rukwa litaundwa na timu za Rukwa yenyewe, Katavi, Kigoma, Tabora, Ruvuma, Songwe na Mbeya. 
    Kundi C litakalokuwa Singida litaundwa na timu za Singida, Dodoma, Iringa, Njombe, Dar es Salaam, Lindi na Mtwara, wakati Kundi D litakalokuwa Kilimanjaro litaundwa na timu za Kilimanjaro yenyewe, Tanga, Arusha, Manyara, Pwani, Morogoro na Dar es Salaam.
    Tukuyu Stars iliweka rekodi ambayo haijavunjwa, kupandwa Ligi Kuu, wakati huo Ligi Daraja la Kwanza na kwenda moja kwa moja kuchukua ubingwa wa ligi hiyo mbele ya vigogo, Simba na Yanga.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TUKUYU STARS KUSHIRIKI LIGI YA MABINGWA WA MIKOA 2018 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top