• HABARI MPYA

  Wednesday, April 04, 2018

  SIMBA SC YAREJEA IRINGA KUWEKA KAMBI TENA KUJIANDAA NA MECHI DHIDI YA MTIBWA JUMATATU

  Na Mwandishi Wetu, IRINGA
  SIMBA SC imeondoka Njombe leo asubuhi kurejea Iringa kuweka kambi ya siku mbili kabla ya kwenda Morogoro kwa mchezo wake ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Mtibwa Sugar Jumatatu ijayo.
  Simba SC jana ilijitanua kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Njombe Mji FC Uwanja wa Saba Saba mjini Njombe.
  Pongezi kwa mfungaji wa mabao hayo yote mawili leo, Nahodha John Raphael Bocco ‘Adebayor’, moja kila kipindi na sasa Wekundi wa Msimbazi wanafikisha pointi 49 baada ya kucheza mechi 21, wakiwazidi kwa pointi tatu mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 43 za mechi 21 pia.  
  Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa chipukizi Meschak Suda kutoka Songea, aliyesaidiwa na Mohamed Mkono wa Tanga, Bocco alifunga bao la kwanza dakika ya 17 na la pili dakika ya 64.
  Ikumbukwe Simba ilikwenda Njombe ikitokea Iringa pia ambako iliweka kambi ya siku mbili kabla ya mchezo huo na leo wanarudi tena mkoani humo kujiandaa na mchezo huo.
  Wekundu wa Msimbazi, wamepania kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2012 ili kurejesha heshima yao.   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAREJEA IRINGA KUWEKA KAMBI TENA KUJIANDAA NA MECHI DHIDI YA MTIBWA JUMATATU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top