• HABARI MPYA

    Monday, April 02, 2018

    SIMBA SC WAIFUATA NJOMBE KIKAMILIFU, JONAS MKUDE YUKO FITI TIMAMU KABISA

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    KIKOSI cha Simba SC kimeondoka leo mjini Iringa kwenda Njombe tayari kwa mchezo wake wa kesho wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania dhidi ya Njombe Mji FC. 
    Simba iliwasili Iringa Jumamosi na kufanya mazoezi kwa siku mbili Uwanja wa Samora kabla ya leo kwenda Njombe tayari kwa mchezo huo wa kiporo.
    Faraja zaidi ni kwamba, kiungo wake Jonas Gerald Mkude alifanya mazoezi jana ni miongoni mwa wachezaji waliosafiri na kikosi kwenda Njombe.
    Simba SC watakuwa wageni wa Njombe Mji FC katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Saba Saba mjini Njombe kesho.
    Mkude aliumia Jumatatu iliyopita kwenye mazoezi ya Simba SC Uwanja wa Boko Veterani mjini Dar es Salaam bada ya kugongana na kiungo mwenzake, Muzamil Yassin wakati wa kugombea mpira – lakini jana alianza mazoezi.
    Simba wanarejea kwenye Ligi Kuu baada ya kutolewa kwenye Kombe la Shirikisho la Afrika na Al Masry ya Misri kwa mabao ya ugenini baada ya sare ya 0-0 Machi 17 mjini Port Said na 2-2 Machi 7, mwaka huu Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam kwenye mchezo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza Kombe la Shirikisho Afrika.
    Simba SC ndiyo wanaoongoza Ligi Kuu kwa wastani wao mzuri wa mabao baada ya kulingana kwa pointi na mabingwa watetezi, Yanga SC 46 kila timu, ingawa pia Wekundu wa Msimbazi wana mechi moja mkononi. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC WAIFUATA NJOMBE KIKAMILIFU, JONAS MKUDE YUKO FITI TIMAMU KABISA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top