• HABARI MPYA

  Thursday, April 05, 2018

  NAHODHA SIMBA SC, JOHN RAPHAEL BOCCO ASEMA; AKILI YETU IPO KWENYE UBINGWA TU

  Na Mwandishi Wetu, NJOMBE
  NAHODHA wa Simba SC, John Raphael Bocco amesema kwa sasa akili zao zipo kwenye ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara wakihitaji kushinda kila mechi ili kutimiza malengo yao hayo.
  Bocco aliyasema hayo baada ya kuisaidia Simba kushinda 2-0 katika mchezo wa ugenini wa Ligi Kuu dhidi ya wenyeji, Njombe Mji FC Jumanne Uwanja w Saba Saba.
  Siku hiyo, mchezaji huyo wa zamani wa Azam FC alifunga mabao yote, moja kila kipindi Simba SC ikipata ushindi mzuri wa ugenini na kujiweka sawa kwenye mbio za ubingwa. 
  Na akizungumza juzi baada ya mchezo huo, Bocco alisema kwamba licha ya kupata ushindi katika mchezo na Njombe lakini hawatabweteka na kuhakikisha wanapambana kupata pointi tatu muhimu.

  John Bocco amesema kwa sasa akili zao zipo kwenye ubingwa wa Ligi Kuu  

  “Tunashukuru kupata pointi tatu muhimu katika mchezo na Njombe, tunasahau na kuelekeza akili zetu katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar," alisema.
  Bocco alisema kikosi chao kipo vizuri kwa ajili ya kupambana na kupata ushindi na kufikia malengo yao ya kutwaa taji la ubingwa wa Ligi Kuu.
  Simba iliondoka Njombe jana asubuhi kurejea Iringa kuweka kambi ya siku mbili kabla ya kwenda Morogoro kwa mchezo wake ujao wa Ligi Kuu dhidi ya wenyeji, Mtibwa Sugar Jumatatu Uwanja wa Jamhuri.
  Kwa sasa Wekundi hao wa Msimbazi ndiyo wanaongoza Ligi Kuu kwa pointi zao 49 baada ya kucheza mechi 21, wakiwazidi kwa pointi tatu mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 46 za mechi 21 pia.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NAHODHA SIMBA SC, JOHN RAPHAEL BOCCO ASEMA; AKILI YETU IPO KWENYE UBINGWA TU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top