• HABARI MPYA

  Thursday, April 12, 2018

  MECHI YA RUVU SHOOTING NA AZAM FC YAAHIRISHWA SABABU YA MVUA, UWANJA UMEJAA MAJI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MCHEZO wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya wenyeji, Ruvu Shooting na Azam FC uliopangwa kufanyika Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani umeahirishwa hadi kesho Saa 10:00 jioni tena.
  Sababu za kuahirishwa kwa mchezo huo ni maji mengi kutuwama kwenye Uwanja wa Mabatini kutokana na mvua kubwa iliyonyesha leo.
  Mechi nyingine mbili za Ligi Kuu zinatarajiwa kuendelea kama kawaida, Simba SC wakiwakaribisha Mbeya City Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam na Mtibwa Sugar wakiwa wenyeji wa Ndanda FC Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.
  Ikumbukwe mechi tano za Ligi Kuu zilichezwa jana kwenye viwanja tofauti, Yanga SC ikilazimishwa sare ya 1-1 na Singida United Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Maji Maji ikiichapa 3-1 Stand United Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
  Nayo Mbao FC ikishinda 2-1 dhidi ya Njombe Mji FC Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, Mwadui FC iliichapa 2-1 Lipuli ya Iringa Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga wakati Tanzania Prisons ililazimishwa sare ya 1-1 na Kagera Sugar Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MECHI YA RUVU SHOOTING NA AZAM FC YAAHIRISHWA SABABU YA MVUA, UWANJA UMEJAA MAJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top