• HABARI MPYA

  Tuesday, April 10, 2018

  MBEYA CITY YAIFUATA SIMBA SC BILA MABEKI WAKE WAWILI TEGEMEO, KABANDA NA MWASAPILI

  Na Princess Asia, MBEYA
  TIMU ya Mbeya City itawakosa mabeki wake tegemeo, John Kabanda na Hassan Mwasapili kwenye mchezo wake wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Simba SC Alhamisi Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
  Baada ya sare ya 0-0 na Azam FC Jumapili Uwanja wa Sokoine mjini, Mbeya City wanasafiri kesho kwenda Dar es Salaam kwa mchezo mwingine wa Ligi Kuu Alhamisi.
  Na kuelekea mchezo huo, Kocha Mkuu wa MCC, Mrundi Ramadhani Nswanzurimo ameiambia Bin Zubeiry Sports - Online kwamba atawakosa Mwasapili ambaye atakuwa anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano na John Kabanda ambaye ni majeruhi.
  Lakini kocha huyo amesema kwamba kukosekana kwa wachezaji hao hakutaiathiri sana timu, kwa sababu nafasi zao zitazibwa na mabeki wengine, Haruna Shamte na Rajab Isihaka.
  "Nitawakosa wachezaji hao wawili, kwa kuwa nina wachezaji wengi ninaimani watachukuwa nafasi zao na kutendea haki," alisema.
  Kocha huyo alisema matokeo ya mechi yao na Azam FC imewapa morali wachezaji wake kuhakikisha wanaenda kupambana kupata pointi kwa Simba.
  "Tunahitaji pointi kwa kila mchezo ili tujiweke katika mazingira mazuri katika msimamo wa ligi, tukilenga pointi nyingine kutoka Simba," alisema Nswanzurimo.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBEYA CITY YAIFUATA SIMBA SC BILA MABEKI WAKE WAWILI TEGEMEO, KABANDA NA MWASAPILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top