• HABARI MPYA

  Friday, April 06, 2018

  LUKAKU AWA MCHEZAJI BORA WA MWEZI MACHI MAN UNITED

  MSHAMBULIAJI Romelu Lukaku amekuwa mchezaji bora wa mwezi Machi wa Manchester United baada ya kupata asilimia 71 ya kura zilizopigwa na mashabiki kupitia akaunti ya Twitter ya klabu hiyo,@ManUtd.
  Mbelgiji huyo, Lukaku amewashinda wachezaji wenzake, Nemanja Matic aliyepata asilimia 22 ya kura na Ashley Young aliyeambulia asilimia saba baada ya kuingia tatu bora.
  Baada ya kuingia kwenye tatu bora za miezi miwili iliyotangulia Septemba na Februari bila mafanikio, hatimaye mwezi huu wa tatu ameondoka na tuzo.
  "Ningependa kuwashukuru mashabiki kwa kunichagua. Wakati wote najaribu kuwalipa fadhila na nitajaribu kufanya hivyom kati ya sasa na mwisho wa msimu,"alisema na kunukuliwa na tovuti ya klabu, ManUtd.com. 

  Romelu Lukaku amekuwa mchezaji bora wa mwezi Machi wa Manchester United 
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LUKAKU AWA MCHEZAJI BORA WA MWEZI MACHI MAN UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top