• HABARI MPYA

  Monday, April 09, 2018

  GOR MAHIA YAKARIBIA KUTINGA MAKUNDI KOMBE LA SHIRIKISHO

  MABINGWA wa Kenya, Gor Mahia wametanguliza mguu mmoja hatua ta makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Supersport United ya Afrika Kusini jana Uwanja wa Machakos.
  Ahsante kwa mfungaji wa bao hilo pekee, mshambuliaji kutoka Rwanda, Jacques Tuyisenge aliyefunga dakika ya 77, Gor wakitarajia kuweka historia ya kucheza hatua ya makundi.
  "Nafikiri tulikuwa vizuri mno leo na kila mmoja alijituma mchezoni. Ninafuraha tumeshinda 1-0 ingawa tulitengeneza nafasi zaidi, lakini tunatakiwa kufanya hivi pia hadi kwenye mchezo wa marudiano mjini Pretoria,” alisema kocha wa Gor Mahia, Muingereza Dylan Kerr baada ya mechi jana.
  Kwa upande wake, kocha wa Supersport, Kaitano Tembo alikuwa vizuri tu licha ya kipigo akibaki na matumaini makubwa ya kupindua matokeo kwenye mchezo wa marudiano.
  "Pongezi kwao, walistahili matokeo haya leo. Ni timu nzuri na wameonyesha hilo. Tulifanya vizuri, lakini nafikiri haya ni matokeo ambayo tunaweza kuyageuza. Tunahitaji kupata vitu vichache tu sahihi, lakini hii mechi bado haijaisha,” alisema Tembo.

  Mshambuliaji kutoka Rwanda, Jacques Tuyisenge (kulia) akishangilia jana baada ya kuifungia bao pekee Gor Mahia

  MATOKEO YA MECHI ZOTE ZA KWANZA  KUFUZU MAKUNDI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA 
  Ijumaa Aprili 6, 2018
  Bidvest (Afrika Kusini) 1-1 Enyimba (Nigeria)
  CF Mounana (Gabon) 1-1 El Masry (Misri)
  Rayon Sports (Rwanda) 3-0 Costa do Sol (Msumbiji)
  Jumamosi Aprili 7, 2018
  Zanaco (Zambia) 0-2 Raja Club Athletic (Morocco)
  AS Vita (DRC) 1-0 CS la Mancha (Kongo)
  Saint George (Ethiopia) 1-0 CARA (Kongo)
  UD Songo (Msumbiji) 3-1 Hilal Obeid (Sudan)
  Plateau United (Nigeria) 2-1 USM Alger (Algeria)
  Yanga SC (Tanzania) 2-0 Wolaitta Dicha (Ethiopia)
  Generation Foot (Senegal) 3-1 RS Berkane (Morocco)
  Williamsville (Ivory Coast) 2-0 Niefang (Equatorial Guinea)
  Jumapili Aprili 8, 2018
  El Hilal (Sudan) vs Akwa United (Nigeria)
  Gor Mahia (Kenya) 1-0 Supersport (Afrika Kusini)
  Aduana (Ghana) 6-1 Fosa Juniors (Madagascar)
  ASEC Mimosas (Ivory Coast) 1-0 CR Belouizdad (Algeria)
  MFM (Nigeria) vs Djoliba (Mali)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GOR MAHIA YAKARIBIA KUTINGA MAKUNDI KOMBE LA SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top