• HABARI MPYA

  Thursday, April 19, 2018

  GOR MAHIA YAITUPA NJE SUPESPORT NA KWENDA MAKUNDI SHIRIKISHO

  MABINGWA wa Kenya, Gor Mahia wamefuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la Afrika licha ya kufungwa mabao 2-1 na wenyeji, Supersport United katika mchezo wa marudiano wa mchujo jana Uwanja wa Lucas Moripe mjini Pretoria, Afrika Kusini.
  Gor Mahia walio chini ya kocha wa zamani wa Simba ya Tanzania, Dylan Kerr raia wa Uingereza wanasonga mbele kwa faida ya mabao ya ugenini kuhesabiwa mara mbili, kufuatia sare ya jumla ya 2-2 baada ya awali kushinda 1-0 mjini Machakos siku 10 zilizotanguli.
  Katika mchezo wa jana, bao la kujifunga la Nahodha wa Gor, Harun Shakava liliipa bao la kwanza Supersport mwanzoni mwa kiopindi cha pili, kabla ya Francis Kahata kuisawazishia timu ya Kenya dakika chache baadaye. 
  Na Thabo Mnyamane akaifungia Supersport United bao la pili dakika ya 68, lakini Gor wakasimama imara kutoruhusu mabao zaidi.
  Baada ya mchezo huo, kocha wa Gor, Kerr alisema; "Nimefarijika sana na nimefurahi kwa mafanikio ya umoja huu wa wachezaji. Tumefanya hivi kwa Gor Mahia, tumefanya hivi kwa soka ya Kenya,”.

  Francis Kahata (kulia) baada ya kuisawazishia Gor Mahia jana dhidi ya Supersport United Uwanja wa Lucas Moripe  

  MATOKEO YOTE MECHI ZA MCHUJO WA KUINGIA HATUA YA MAKUNDI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA
  Jumanne Aprili 17, 2018
  CS la Mancha (Kongo) 1-5 AS Vita (DRC) (0-1)
  USM Alger (Algeria) 4-0 Plateau United (Nigeria) (1-2)
  El Masry (Misir) 2-1 Mounana (Gabon) (1-1)
  CR Belouizdad (Algeria) 0-0 ASEC Mimosas (Ivory Coast) (0-1)
  Jumatano, Aprili 18, 2018
  Raja Club Athletic (Morocco) 3-0 Zanaco (Zambia) (2-0)
  CARA (Kongo) 1-0 (4-3pen) Saint George (Ethiopia) (0-1)
  Akwa United (Nigeria) 3-1 El Hilal (Sudan) (0-2)
  Supersport (Afrika Kusini) 2-1 Gor Mahia (Kenya) (0—1)
  Hilal Obied (Sudan) 2-1 UD Songo (Msumbiji) (1-3)
  Enyimba (Nigeria) 0-0 Bidvest (Afrika Kusini) (1-1)
  Fosa Juniors (Madagascar) 2-1 Aduana (Ghana) (1-6)
  Wolaitta Dicha (Ethiopia) 1-0 Yanga SC (Tanzania) (0-2)
  RS Berkane (Morocco) vs Generation Foot (Senegal) (1-3)
  Niefang (Equatorial Guinea) 2-1 Williamsville (Ivory Coast) (0-2)
  Djoliba (Mali) vs MFM (Nigeria) (1-0)
  Costa do Sol (Msumbiji) 2-0 Rayon Sports (Rwanda) (0-3)
  TIMU ZOTE ZILIZOFUZU; 
  AS Vita (DRC), USM Alger (Algeria), El Masry (Misir), CARA (Kongo), El Hilal (Sudan), Gor Mahia (Kenya), UD Songo (Msumbiji), Enyimba (Nigeria), Aduana (Ghana), Yanga SC (Tanzania), RS Berkane (Morocco), Williamsville (Ivory Coast), Djoliba (Mali), Rayon Sports (Rwanda), Raja Club Athletic (Morocco)  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GOR MAHIA YAITUPA NJE SUPESPORT NA KWENDA MAKUNDI SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top