• HABARI MPYA

  Thursday, January 18, 2018

  WALAAL MUSA AIPELEKA SUDAN ROBO FAINALI CHAN 2018

  MSHAMBULIAJI Walaal Musa jana alikuwa shujaa wa Sudan baada ya bao lake pekee katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Mauritania kuipeleka timu yake Robo Fainali ya Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN).
  Ushindi huo unawafanya Desert Hawks wafuzu Nane Bora wakiungana na wenyeji, Morocco ambao katika mchezo uliotangulia jana waliichapa Guinea 3-1 at Uwanja wa Mohamed V mjini Casablanca.
  Sasa Morocco na Sudan kila timu ina pointi sita katika Kundi A, mbele ya  Guinea na Mauritania ambazo hazina pointi.
  CHAN inaendelea leo kwa mechi za Kundi B, Ivory Coast ikimenyana na Zambia na Uganda watacheza na Namibia. 
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WALAAL MUSA AIPELEKA SUDAN ROBO FAINALI CHAN 2018 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top