• HABARI MPYA

  Saturday, January 20, 2018

  STAND UNITED YAIBWAGA MBAO FC 1-0 KIRUMBA, NJOMBE MJI YAIKATALIA MTIBWA MANUNGU

  Na Mwandishi Wetu, MWANZA
  TIMU ya Stand United imewazima Mbao FC kwa kuwachapa bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.
  Ushindi huo unaifanya Stand United ifikishe pointi 13 baada ya kucheza mechi 14 na kusogea juu hadi nafasi ya 11 kutoka mkiani kwenye ligi ya timu 16.
  Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Jacob Adongo aliyesaidiwa na Hellen Mduma na Martin Mwalyaje, Stand United walipata bao lao dakika ya 40.
  Bao hilo lilifungwa na mshambuliaji Vitalis Mayanga kwa penalti baada ya kipa wa Mbao FC, Ivan Rugumandiye kumkamata miguu Landry Ndikumana baada ya wote kuanguka wakati wanawania mpira kwenye boksi.
  Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Mtibwa Sugar imelazimishwa sare ya 0-0 na Njombe Mji FC Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro. 
  Kikosi cha Mbao FC kilikuwa; Ivan Rugumandiye, Vincent Philipo, Amos Abel, David Mwasa, Yusuph Ndikumana, Ibrahim Njohole/Ismail Ally dk75, James Msuva, George Sangija, Habib Kiyombo/Robert Ndaki dk81, Emmanuel Mvuyekure na Abubakar Mfaume/Abdul Segeja dk55.
  Stand United; Mohamed Makaka, Makenzi Ramadhani, Miraj Maka, Ally Ally, Erick Mulilo, Ismail Gambo, Abdul Kassim, Bigirimana Babikakuhe, Abdallah Juma/Ally Khamisi dk75, Ndikumana Landry na Vitalis Mayanga.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: STAND UNITED YAIBWAGA MBAO FC 1-0 KIRUMBA, NJOMBE MJI YAIKATALIA MTIBWA MANUNGU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top