• HABARI MPYA

    Thursday, February 26, 2026

    TRA UNITED YAICHAPA FOUNTAIN GATE 4-1 KARATU

    Mshambuliaji wa TRA United, Enock Jiah Mkanga amekuwa Mchezaji Bora wa Mechi baada ya kufunga mabao mawili leo 

    TIMU ya TRA United imeibuka na ushindi wa mabao 4-1 shida ya Fountain Gate katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Black Rhino Sports Complex, Karatu mkoani Arusha.
    Mabao ya TRA United leo yamefungwa na mshambuliaji, Enock Jiah Mkanga mawili dakika ya 29 na 56, Amy Mapaka dakika ya 45 na beki Mzambia, Chanda Chewe dakika ya 51, wakati bao pekee la Fountain Gate limefungwa na mshambuliaji Mnigeria, Chukwunonye Obasi dakika ya 83. 
    Kwa ushindi huo, TRA United inafikisha pointi 16 katika mchezo wa 13 na kusogea nafasi ya 10 kutoka ya 12, wakati Fountan Gate inabaki pointi zake 12 za mechi 14 sasa nafasi ya 15 kwenye Ligi ya timu 16.
    Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja na mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
    Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu kutoka Ligi ya Championship katika mechi nyingine mbili za mchujo nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TRA UNITED YAICHAPA FOUNTAIN GATE 4-1 KARATU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top