• HABARI MPYA

  Saturday, January 20, 2018

  SERGI ROBERTO AJITIA KITANZI BARCELONA MIAKA MINNE NA NUSU

  KIUNGO Sergi Roberto amezima tetesi zote za kuondoka Barcelona baada ya kukubali kusaini mkataba mpya wa miaka minne na nusu kuendelea kufanya kazi Nou Camp.
  Roberto amekuwa akihusishwa na kwenda kuungana tena na kocha wake zamani, Pep Guardiola ambaye kwa sasa yupo Manchester City, lakini kocha wa Barcelona, Ernesto Valverde amehakikisha mhitimu huyo wa akadeki ya timu anasaini mkataba wa muda mrefu.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ambaye amecheza mechi 25 msimu huu, alikuwa amebakiza miezi 18 katika mkataba wake wa sasa wenye thamani ya Pauni Milioni 35.

  Sergi Roberto amesaini mkataba mpya wa kuendelea kutumika Barcelona PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  Pamoja na hayo, mwanasoka huyo wa kimataifa wa Hispania sasa anabaki na vinara hao wa La Liga hadi Juni 2022 na timu itakamyomhitaji itamnunua kwa Pauni Milioni 440.
  Roberto amekuwa na bahati ya kushinda mataji na klabu hiyo tangu apandishwe kikosi cha kwanza Novemba mwaka 2010.
  Ameshinda mataji manne ya La Liga, mawili ya Ligi ya Mabingwa na manne ya Kombe la Mfalme, au Copa del Rey na anakuwa mchezaji wa pili wa Barca kuongeza mkataba wiki hii, baada ya beki Gerard Pique ambaye alisaini mkataba mpya Alhamisi utakaomuweka Camp Noo hadi mwishoni mwa msimu wa 2021/2022.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SERGI ROBERTO AJITIA KITANZI BARCELONA MIAKA MINNE NA NUSU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top