• HABARI MPYA

  Saturday, January 20, 2018

  YANGA SC YATAJA SABABU ZA BEKI MPYA MKONGO KUTOONEKANA

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  BEKI mpya wa Yanga, Mkongo Fiston 'Festo' Kayembe Kanku ameshindwa kujiunga na timu tangu asajiliwe Desemba kutokana na matatizo ya kifamilia.
  Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Hussein Nyika katika mahojiano maalum na Bin Zubeiry Sports – Online leo mjini Dar es Salaam.
  Nyika amesema kwamba Kanku tayari ni mchezaji wa Yanga na atajiunga na timu mara atakapomaliza matatizo yake ya kifamilia.
  “Kanku ana matatizo ya kifamilia na ni makubwa ndiyo maana tumemruhusu kwa sasa aende kuyashughulikia, akimaliza atakuja kuanza kazi, na muda upo, Ligi bado mbichi sana,”amesema Nyika.
  Fiston 'Festo' Kayembe Kanku ameshindwa kujiunga na timu tangu asajiliwe Desemba kutokana na matatizo ya kifamilia

  Lakini pia, Nyika amesema kwamba uhamisho wake wa kimataifa (ITC) nao pia ulikuwa unasumbua ila kwa sasa wapo kwenye hatua za mwisho kuupata.  
  Baada ya kuwa majaribio tangu Agosti, Kanku alisaini mkataba wa miaka miwili Desemba mwaka jana na kuzima kabisa uwezekano wa beki Mtogo, Vincent Bossou kurejeshwa Jangwani, licha ya kupigiwa debe na wadau mbalimbali wa klabu hiyo, arejeshwe kikosini.
  Bossou alimaliza mkataba wake msimu uliopita baada ya kuitumikia Yanga kwa miaka miwili alitarajiwa kuendelea kutokana na kufanya vizuri, lakini klabu haikumpa mkataba mpya baada ya mazungumzo ya muda mrefu.
  Ilifikiriwa hali mbaya ya kiuchumi ilisababisha Yanga kumwaka kumpa mkataba mpya Bossou, lakini kitendo cha klabu kumsajili Kayembe anayetokea Balende FC ya kwao, Jamhuri ya Kidemkrasia ya Kongo (DRC) kinaashiria imeamua kuachana na Mtogo huyo kwa vyovyote.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YATAJA SABABU ZA BEKI MPYA MKONGO KUTOONEKANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top