• HABARI MPYA

  Friday, January 19, 2018

  MBEYA CITY YAFIKISHA MECHI SABA BILA USHINDI, SARE MBILI TU NYINGINE ZOTE WAMEPIGWA

  MARA YA MWISHO MBEYA CITY KUSHINDA
  Oktoba 21, 2017; Mbeya City 2-0 Ruvu Shooting
  REKODI YA MBEYA CITY KUTOSHINDA
  Oktoba 27, 2017; Azam FC 1-0 Mbeya City
  Novemba 5, 2017; Mbeya City 0-1 Simba
  Novemba 19, 2017; Yanga SC 5-0 Mbeya City
  Novemba 25, 2017; Singida United 2-1 Mbeya City
  Januari 2, 2018; Mbeya City 0-0 Kagera Sugar
  Januari 14, 2018; Tanzania Prisons 3 -2 Mbeya City
  Januari 19, 2018; Mbeya City 0-0 Lipuli FC
  Kocha Mrundi wa Mbeya City, Ramadhani Nswazurino amekalia kuti kavu

  Na Mwandishi Wetu, MBEYA

  TIMU ya Mbeya City imeendelea na mwendo wa kusuasua katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya leo kulazimishwa sare ya 0-0 na Lipuli ya Iringa Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
  Matokeo hayo, yanaiongezea pointi moja Mbeya City ambayo sasa ni timu binafasi baada ya kutemwa na Halmashauri ya Jiji la Mbeya ikifikisha pointi 13 baada ya kucheza mechi 14 na kupanda hadi nafasi ya 10, wakati Lipuli inayofikisha pointi 15 katika mechi ya 14 pia, inabaki nafasi ya nane. 
  Leo Mbeya City inayofundishwa na kocha Mrundi, Ramadhani Nswazurino imefikisha mechi saba za kucheza bila kushinda, ikitoa sare ya pili na kufungwa mechi tano tangu Oktoba 27, mwaka jana.
  Mara ya mwisho Mbeya City kushinda ilikuwa ni Oktoba 21, mwaka jana ilipoichapa Ruvu Shooting 2-0 na baada ya hapo ikafungwa 1-0 mfululizo na Azam FC Oktoba 27 Dar es Salaam na Simba SC Novemba 5 Mbeya kabla ya kuchapwa 5-0 na Yanga Novemba 19 Dar es Salaam.
  Mechi nyingine, MCC ilifungwa 2-1 na Singida United Novemba 25 Singida, ikatoka sare ya 0-0 na Kagera Sugar Januari 2, mwaka 2018, ikafungwa 3-2 na Tanzania Prisons Januari 14, kabla ya sare ya leo zote nyumbani, Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
  Ligi Kuu itaendelea kesho kwa mechi nne zaidi, Uwanja w CCM Kirumba mjini Mwanza Mbao wataikaribisha Stand United, Mtibwa Sugar wataikaribisha Njombe Mji Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro, Tanzania Prisons watakuwa wenyeji wa Azam FC Uwanja wa Azam Complex na Mwadui FC wataikaribisha Ndanda FC Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga.
  Jumapili kutakuwa na mchezo mmoja tu, mabingwa watetezi, Yanga SC wakimenyana na Ruvu Shooting Uwanja wa Taifa wakati mzunguko wa 14 utakamilishwa Jumatatu kwa mechi mbili, Kagera Sugar wakiikaribisha Simba SC Uwanja wa Kaitaba na Maji Maji wakiwa wenyeji wa Singida United Uwanja wa Maji Maji mjini Songea.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBEYA CITY YAFIKISHA MECHI SABA BILA USHINDI, SARE MBILI TU NYINGINE ZOTE WAMEPIGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top