• HABARI MPYA

  Friday, January 19, 2018

  HANS POPPE AAHIDI KUMNUNULIA GARI NDEMLA, AMUAMBIA ACHAGUE LOLOTE ATAKALO

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe ameahidi kumnunulia gari kiungo wa klabu hiyo, Said Hamisi Ndemla.
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo mjini Dar es Salaam, Poppe amesema kwamba huo ni utaratibu wa kawaida aliohjiwekea wa kuwazawadia gari wachezaji wanaojituma na wenye nidhamu kwenye timu.
  “Yeye mwenyewe atachagua gari yoyote aipendayo, mimi nitamnunulia. Bado sijainunua nimempa ahadi tu ambayo nitaitekeleza mara moja,”amesema Hans Poppe, Kapteni wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ). 
  Kiungo wa Simba SC, Said Hamisi Ndemla ameahidiwa gari na Zacharia Hans Poppe

  Ndemla atakuwa mchezaji wa pili Simba kuzawadiwa gari na Poppe baada ya beki, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ kupewa gari aina ya Toyota Raum Septemba mwaka 2016  
  Na Hans Poppe amesema amevutiwa na Ndemla kutokana na nidhamu yake na kujituma bila kukata tama wakati wote.
  “Ni mchezaji ambaye hana neno anapokuwa hapangwi, na akiinuliwa kuingia uwanjani wakati wowote huenda kufanya vizuri na kuisaidia timu. Kwa kweli huyu kijana ni mfano wa kuigwa kwe wenzake na anastahili zawadi hii,”amesema.
  Poppe amesema kwamba utamadunia wa kuwazawadia gari wachezaji wa klabu yake hiyo utaendelea na jukumu la kila mchezaji kuonyesha nidhamu na bidii kama Ndemla.   
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HANS POPPE AAHIDI KUMNUNULIA GARI NDEMLA, AMUAMBIA ACHAGUE LOLOTE ATAKALO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top