• HABARI MPYA

  Monday, January 15, 2018

  AZAM FC WAUNGANISHA SONGEA KUIFUATA MAJI MAJI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MARA baada ya kutwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi jana, kikosi cha Azam FC leo asubuhi kimeondoka Dar es Salaa kwenda mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kucheza mechi mbili mfululizo za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL).
  Jumamosi Azam FC ilitwaa ubingwa wa nne wa Kombe la Mapinduzi baada ya kuichapa URA ya Uganda kwa mikwaju ya penalti 4-3 kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 90.
  Na kikosi cha timu hiyo kilirejea jana mchana mjini Dar es Salaam kwa mapumziko mafupi kabla ya leo kuanza safari nyingine.
  Msafara wa Azam FC uliokuwa ukiongozwa na  na Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdul Mohamed na Makamu Mwenyekiti, Abdulkarim Amin ‘Popat’, ulipokewa na mamia ya mashabiki waliojitokeza bandarini kwa shangwe kubwa kwa furaha.
  Wachezaji Waghana wa Azam FC, kipa Razack Abalora (kulia) na winga Enock Atta Agyei
  Ikiwa katika mikoa hiyo miwili ya Nyanda za Juu Kusini, Ruvuma na Mbeya, Azam FC itacheza mechi mbili dhidi ya Maji Maji mjini Songea Alhamisi wiki hii Saa 8.00 mchana huku ikimalizia mtihani wa mwisho Januari 22 kwa kukipiga na Tanzania Prisons Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya saa 10.00 jioni.
  Azam FC itaendelea kumkosa mshambuliaji wake, Mbaraka Yusuph ambaye alikuwa majeruhi na ataungana na timu itakaporejea kutoka Nyanda za Juu kusini.
  Azam FC inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu kwa pointi zake 26 sawa na vinara, Simba SC walio juu kwa wastani wao mzuri wa mabao.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC WAUNGANISHA SONGEA KUIFUATA MAJI MAJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top