• HABARI MPYA

    Monday, January 22, 2018

    ARSENAL WATUA UJERUMANI KUMALIZANA NA DORTMUND WAMCHUKUE AUBAMEYANG

    KLABU ya Arsenal imepiga hatua katika kuwania saini ya mshambuliaji Pierre-Emerick Aubameyang baada ya Mtendaji wake Mkuu, Ivan Gazidis na Mkuu wa Usajili, Sven Mislintat kuonekana wakiwasili nchini Ujerumani jana kwa mazungumzo ya uso kwa uso.
    Gazidis na Mislintat walipigwa picha wakiwasili kwa mkutano na viongozi wa Borussia Dortmund, akiwemo Mtendaji wao Mkuu, Hans-Joachim Watzke na Meneja Mkuu, Michael Zorc. 
    Wawili hao wa Dortmund walitokea vizuri kwenye picha kuliko wenzao wa Arsenal – kuashiria kwamba wanafahamu kiasi gani wao ndiyo wameshikilia mpini wa siku kwenye mazungumzo hayo. 


    Arsenal executive Ivan Gazidis and head of recruitment Sven Mislintat arrive for talks PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

    Tayari Dortmund imekataa ofa ya kwanza ya Arsenal ya Pauni Milioni 44 na inaelekea The Gunners wamedhamiria kumng'oa Aubameyang Signal Iduna Park kwa kuwasilisha ofa ya Pauni Milioni 53.  
    Mshambuliaji aliachwa nje ya kikosi kilichotoa sare ya 1-1 na Hertha Berlin wakati klabu ikishughulikia uhamisho wa nyota huyo wa Gabon.
    Arsenal wameongeza bidii kuhakikisha wanampata mchezaji huyo kutokana na wao mshambuliaji wao tegemo, Alexis Sanchez kuwa mbioni kujiunga na Manchester United kuwa kubadilishana na kiungo Henrikh Mkhitaryan. 
    Mshambuliaji huyo wa Gabon ghafla amejikuta katika maisha magumu klabu hiyo ya Bundesliga baada ya kusimamishwa zaidi ya mara moja katika mzunfuko wa kwanza. 
    Akiwa amefunga mabao 21 kwenye mashindano yote hadi sasa msimu huu, Arsene Wenger anataka kumchukua Aubameyang ahamishie makali yake Uwanja wa Emirates zikiwa zimebaki siku 10 kaba ya days dirisha dogo la usajilo kufungwa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ARSENAL WATUA UJERUMANI KUMALIZANA NA DORTMUND WAMCHUKUE AUBAMEYANG Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top