• HABARI MPYA

  Monday, January 22, 2018

  ALEXIS SANCHEZ NI WA MANCHESTER UNITED KUANZIA SASA

  Manchester United imetangaza kumsajili mshambuliaji Alexis Sanchez kutoka Arsenal, zote za England PICHA ZAIDI GONGA HAPA  


  NAMNA SANCHEZ ATAPATA PAUNI 600,000 KWA WIKI MAN UTD 

  Mshahara wa wiki: Pauni 350,000. 
  Hiki ni kiwango cha juu zaidi cha mshahara kwa mchezaji yeyote wa Ligi Kuu. Manchester United ina wachezaji wanne katika sita wanaolipwa mishahara mikubwa zaidi kwa wiki, huku Paul Pogba akipokea Pauni 290,000, Romelu Lukaku on 250,000 na Zlatan Ibrahimovic 220,000. Sergio Aguero na Yaya Toure wa Manchester City pia wanapata Pauni 220,000 kwa wiki.
  Haki za matumizi ya picha Pauni 100,000 kwa wiki
  Na posho Pauni 144,000 kwa wiki
  KLABU ya Manchester United imekamilisha uhamisho wa mshambuliaji Alexis Sanchez kwa mkataba wa miaka minne na nusu kutoka Arsenal na Henrikh Mkhitaryan anakwenda upande wa pili.
  Akiuzungumzia uhamisho wake, Alexis Sanchez amesema: "Nina furaha kujiunga na klabu kubwa duniani. Nimekuwa Arsenal kwa miaka mitatu na nusu mizuri na imenipa kumbukumbu nzuri klabu hiyo kubwa na mashabiki wake.
  "Nafasi ya kucheza kwenye Uwanja huu wa kihistoria na kufanya kazi na Jose Mourinho ni ambayo nisingeweza kuikataa. Ninayo furaha kuwa mchezaji wa kwanza wa Chile kuchezea timu ya kwanza ya United na ninatumai ninaweza kuwaonyesha mashabiki wetu dunia nzima kwa nini klabu imenileta hapa,".
  Jose Mourinho kwa upande wake amesema: "Alexis ni mmoja wa washambuliaji bora duniani na tutakamilisha safu yetu ya ushambuliaji ya wachezaji chipukizi na wenye vipaji. Ataleta matarajio yake, dhamira na haiba, sifa ambazo zimemfanya awe mchezaji wa Manchester United na mchezaji ambaye anaifanya timu iwe madhubuti na mashabiki wajivunie timu yao,".
  "Ningependa kumtakia kila la heri Henrikh, mafanikio yote na furaha ambayo nina uhakika anakwenda kuipata. Ni mchezaji ambaye hatutamsahau, hususan kutokana na mchangi wake kwenye ushindi wa taji letu la Europa League,"amesema.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ALEXIS SANCHEZ NI WA MANCHESTER UNITED KUANZIA SASA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top