• HABARI MPYA

  Friday, December 15, 2017

  YANGA WAIFUATA SIMBA KWENYE MABADILIKO…MCHAKATO WAANZA JANGWANI

  Na Salma Suleiman, DAR ES SALAAM
  BAADA ya uongozi wa klabu ya Simba kutangaza kuingia kwenye mabadiliko ya uendeshaji wa klabu hivi karibuni, Watani wao wa Jadi, Yanga nao leo hii wametangaza kuingia kwenye mfumu huo kwa ajili ya maendeleo ya soka la kisasa.
  Akizungumza na Wanahabari leo kwenye makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo Mtaa wa Twiga na Jangwani, Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa amesema kwamba Desemba 13 kulikuwa na kikao cha Kamati ya Utendaji ambacho kilijadili ajenda mbalimbali.
  Amesema, moja ya ajenda hizo ni kamati hiyo kuamua klabu iingie kwenye mfumo mpya wa uendeshaji wa kuruhusu kuingiza kwa mwekezaji kwa ajili ya kuendesha.
  Mkwasa amesema kulingana na Katiba yao ya mwaka 2010, Ibara 56 kipengele cha 3 kinajieleza kuwa wanachama wanatakiwa kumiliki hisa 51 na 49 inayobaki inaweza kwenye kwa Mwekezaji.
  “Kikao hicho halali cha Kamati ya Utendaji kiliridhia na kupitia klabu kuingia kwenye mfumo wa mabadiliko kwani kwa sasa ni lazima kuendesha klabu kwa mfumo unaokwenda na wakati,” alisema Mkwassa.
  Aliongeza kuwa, Makamu Mwenyekiti, Clement Sanga atatangaza mchakato mzima wa kuanza kwa mfumo huo na klabu ya kuanza zoezi hilo uongozi wa Yanga utafanya tathmini ya (Assert) za klabu ili kujua zina thamani gani.
  “Yanga ina (Assert) nyingi zikiwemo zinazohamishika kama magari, samani za ofisini na vitu vingine na zile zisizohamishika kama ardhi, hivyo baada ya zoezi hilo ndipo tutatangaza thamani ya klabu yetu kwani hatuwezi kusema tu klabu inasthamani kadhaa bila kujua thamani halisi,” alisema Mkwassa.
  Alisisitiza kuwa, hayo ni mabadiliko ya kweli, huru na ya wazi kwani ikumbukwe kuwa Yanga ndio walikuwa wa kwanza katika jambo hilo.
  “Wanachama hawahitaji historian a wanahitaji matokeo, kwa sasa tutapokea maombi mbalimbali ya wawekezaji na baadaye tutakwenda kwenye mkutano Mkuu wa Wanachama ndani ya miezi mitatu ijayo kwa ajili ya kuwauliza iwapo watakubalina na suala hilo,” amesema Mkwasa.
  Wakati huo huo Mkwasa amesema kwamba katika kuboresha Kamati ya Mashindano, wameamua kuongeza nguvu ambapo Kamati ya utendaji imeunganishwa na Kamati ya Usajili na ile ya Mashindano kwa ajili ya michuano ya Ligi na ile ya Ligi ya Mabingwa.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA WAIFUATA SIMBA KWENYE MABADILIKO…MCHAKATO WAANZA JANGWANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top